Jana
hii picha ilizua mjadala mahali. Mjadala wenyewe ni "Ikulu yetu
imefikia huku?". Maana yake ni kwamba iweje @mubah5 ambaye ni kinyozi
ameweza kuhudhuria dhifa ya kuapishwa Raisi. Nikalala nikiwaza kwamba
imekuwaje? Mimi sikuwa na mualiko. Aidha kwa sababu sikuutafuta au
sikuwa na bahati ya kualikwa. Aidha way sio tatizo. Lakini kwa @mubah5
kualikwa au kuutafuta mualiko kuna maana mbili. Ya kwanza
ni kwamba kama kijana ambaye amejiajiri kwa kazi ya saluni ameweza
kupambana mpaka kufikia kugusana mabega na 'watu muhimu' nchini kwetu.
Kwa kijana ni jambo la kupongeza sio kukebehi. Maana ya pili ni kwamba
Ikulu au dhifa za Ikulu sio kwa ajili ya matajiri na sisi tunaojiona ni
bora kuliko wengine. Kila mtanzania anayo haki ya kualikwa na
kuhudhuria. Hii ni sifa na ndivyo inatakiwa iwe hivyo. Mara nyingi
tumesikia makelele kwamba Ikulu ni ya matajiri na watu fulani! Masikini
na wanyonge haiwahusu. Sasa kwa nini tuhoji kinyozi kijana @mubah5
kuhudhuria? Siamini kwamba masikini na 'mtu anayeonekana sio wa muhimu'
kwenda Ikulu ni tatizo. Wako wengi ni wezi na wadhalimu wanajidai bora
wanaenda na ndio wanaoshiriki kuiba au kufanya biashara haramu!! Ni heri
masikini na mnyonge aende kuliko tajiri mwizi na dhalimu. Mwisho, kuna
watu ambao ni muhimu na bora walialikwa lakini hawakwenda!! Wengine
walisusa na kuona haina sababu. Ndivyo maisha yalivyo. Kwa wale wenye
kusoma Biblia tukumbuke waliokusanywa kwenye kona za mji kuhudhuria
sherehe walikuwa kina nani!! Leo ni siku ya kwanza ya Mh. Dr Magufuli
ofisini. Tuone siku 100 za mwanzo zitatupa muelekeo gani! Ameanza na
uteuzi wa Mwanasheria Mkuu... #HongeraMubah #TanzaniaKwanza #UmojaWetu #AlbertoForPresidency2025 #AlbertoForParliament2020 #KijanaPambana #KijanaOnaFursa #KuwaBora #HeshimuKaziYako @paulmakonda @paulmakonda
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment