mwanazuoni

MITUMBA KUPIGWA MARUFUKU AFRIKA MASHARIKI

Mitumba kupigwa marufuku Afrika Mashariki

 

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokutana leo mjini Arusha, Tanzania wameamua kupiga marufuku uagizaji wa nguo za viatu kuu vya mitumba.
Utekelezaji wake utakuwa baada ya miaka mitatu.
Marufuku hiyo ni moja ya hatua zilizopendekezwa ilikuinua viwanda vya nguo katika kanda ya Afrika Mashariki.
Serikali za Afrika Mashariki zimekuwa zikilaumu uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kama moja ya sababu zinazofanya viwanda vya nguo na ngozi kusambaratika na hivyo kuwanyima wenyeji nafasi ya ajira.
  
 
Nguo za mitumba hutegemewa sana na watu wa mapato ya chini
Nguo hizo hutegemewa sana na watu wenye mapato ya chini kutokana na bei yake nafuu.
Kadhalika, wauzaji wa nguo hizo wasafirishaji,waagizaji wote huzitegemea kupata mkate wao wa kila siku hii ikichangia pato la nchi na ajira kwa maelfu ya watu ambao huhudumu katika biashara hiyo.
Viongozi hao pia watajadili pendekezo la kupunguza kiasi cha magari yaliyotumika yanayoingizwa kanda hii.
Lengo lao likiwa kutafuta mbinu ya kusaidia viwanda vya utengenezaji magari vinavyoendesha biashara Afrika Mashariki.
Marais Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya) na Yoweri Museveni (Uganda) walihudhuria mkutano huo mjini Arusha.
M
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment