Ubunge ni kazi ya wito
katika kuwatumikia wananchi kwa lengo la
kuleta maendeleo na usawa wa haki katika
jamii husika. Na kwa kawaida kiongozi mzuri ni Yule anayefahamu matatizo ya
watu wake na kuyafanyia kazi kwa wakati mahsusi bila ya kusubili kuambiwa.
Kwa kulitambua hilo
mbunge wa Masasi Ndugu Dr Rashid
Chuachua Jana alifanya mkutano wake wa kwanza katika kata ya Mkuti na wapili
tangua achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo
hilo la Masasi. Kwa siku zake 48 za Ubunge ameweza kungundua changamoto
mbalimbali ndani ya jimbo lake hilo na ameanza kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha
anaondoa changamoto hizo.
Suala la Elimu
Mbunge kwa kutambua
mchango wa elimu katika jamii yeyoyote ile katika kuleta maendeleo katika
jamii. Ameweza kufatilia suala la madeni ya walimu pia ni miaka kadhaa sasa
serikali aijapeleka walimu wa shule za msingi hivyo kuna uhaba wa walimu 219. Ila
amefanya mazungumzo na waziri husika na ameaindiwa kupatiwa walimu wote 219 na
serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Changamoto za afya
katika hospitali ya Mkomaindo.
Kuna changamoto nyingi
sana katika hospitali ya Mkomaindo. Kwa kutambua umuhimu wa afya mbunge
amefanya ziara kabla ya kuapishwa kuwa mbunge na kungundua changamoto mbalimbali
zikiwemo ukosefu wa viafa tiba, shuka,
upungufu wa dawa na pia uhaba wa wauguzi katika hospitali hiyo.
Hivyo mbunge alianza
kwa kutoa shuka 690 kwa ajili ya wagonjwa.
Pia Changamoto ya
kukosa kituo cha afya , hivyo mbunge kushirikiana na mganga mkuu wanaandaa
utaratibu wa kuhakikisha wanaborosha zahati ya mkuti.
Kifupi mbunge aligusia
sehemu zote ambazo ni kero kwa wananchi wa jimbo lake pia aliambatana na wakuu
wa Idara zote za Halmashauri ya Masasi pia wakiwemo madiwani na Mwenyekiti wa
Halmashauri kwa lengo la kujibu kero za wananchi na kutolea ufafanuzi juu ya
maswala ambayo ni vikwazo vya maendeleo mbele ya jamii husika.
|
MWANANCHI AKITOA KERO YAKE KUHUSU TAKATAKA |
|
Ndugu Pascal Mratibu CHF akitoa maelezo kuhusu CHF |
|
Wananchi wakifatilia mkutano |
|
Mbunge akibadilishana mawazo wa mwenyekiti wa Halmashauri |
|
Mbunge akiandika swali liloulizwa |
|
MGANGA MKUU AKITOA ELIMU YA MFUKO WA AFYA WA JAMII |
|
Afisa wa Maji akielezea Mikakati |
|
Mbunge akipasua jipu la Chama cha Ushirika MAMCU akiwataka TAKUKURU Kufanya Uchuguzi wa Kina |
|
Mbunge Dr Chuachua akimuagize Mganga mkuu wa Hospital ya Mkomaindo kufatilia waliokuwa wanagawa Neti na Kuwauzia wenye Nyumba za Kulala wageni badala ya kuwapa wananchi hili wachukuliwe hatua |
|
wananchi wakifatilia mkutano |
|
Diwani wa Mkuti Ndugu Nachuma(chadema) |
|
KATIBU WA MBUNGE |
Mtani
Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
0 comments:
Post a Comment