Thomas Isidore Noël Sankara taa ya Afrika iliyozimika ghafla!
Na; Martin Maranja Masese,
Mnamo august 1983, vijana wawili, makapteni wa jeshi na wanamapinduzi,
Thomas Sankara na Blasius Compaore, waliipindua serikali ya Rais wa
wakati huo katika nchi iliyokuwa ikijulikana kama Upper volta, rais huyu
aliitwa Baptiste Ouedraogo...
Vijana hawa wakiwa katika fikra za
Karl Max, wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga Upper volta.., walibadili
kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina
faso, manake nchi ya watu, country of honorable citizen..
Uchapa
kazi wa vijana hawa (Sankara na Compaore), Thomas sankara akiwa ndiye
rais unaweza kufananishwa na ule wa Fider Castrol na Che Guavera, kabla
haujachuja kule Cuba..
Haiyumkini Sankara alikuwa anatumia
baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo, wakati pacha wake
(Compaore) wakiwa kama pete na kidole..
Urafiki wa makapteni hawa
wa jeshi la Burkinabe, ulikuwa mkubwa kiasi ambacho, wakati wanausalama
walipomwambia Sankara kuwa Compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua,
yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, labda mtu
mwingine...
Blaise Compaore alikutana na Thomas Sankara mwaka
1976 katika mafunzo ya kijeshi Morocco na hapo walianza urafiki wao
uliokuwa wazi kwa karibu watu wote waliokuwa wakiwafahamu nchini Burkina
Fasso na nchi jirani.
Thomas Sankara alikuwa akiwaeleza wanausalama wake kuwa, hata kama Compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia.
Ni wazi kuwa Kapteni Thomas Isidore Sankara alikuwa karibu sana na
Blaise Compaore, kwa kiasi ambacho Blaise Compaore alikuwa sehemu ya
maisha ya kila siku ya Sankara...
kama ilivyotabiriwa na watu
wengi wa karibu wa Thomas Sankara, Blaise Compaore aliongoza mapinduzi
yaliyosababisha kifo cha Sankara mnamo mwaka 1987, na yeye mwenyewe
(Compaore), huku akishuhudia rafiki yake kipenzi Sankara akiuuwa, Akawa
ndiye mrithi wa kiti cha Urais wa iliyokuwa Upper Volta baadaye Burkina
Fasso..
Thomas Isidore Noël Sankara ni nani??
Isidore
Noël Thomas Sankara alizaliwa tarehe 12.12.1949 Mjini YOKO katika nchi
iliyokuwa ikiitwa Upper Volta (Volta ya juu) na kuuawa tarehe 15.10.1987
na wanajeshi wenzake wakiongozwa na rafiki yake Rais Blaise Compaore
katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou akiwa katika
kikao cha utendaji wa kazi...
Thomas Sankara alipanda ngazi za
kijeshi hadi cheo cha kaptenu pamoja na mwanajeshi Rafiki yake Blaise
Compaore ANAYEJUA SIRI YA KIFO CHA CHA THOMAS SANKARA .
Kuna
nyakati ambazo Blaise Compaore alipata kunena kwa kinywa chake katika
shirika la kutetea haki za Binadamu duniani kwamba “kifo cha Thomasi
Sankara kilikuwa ni ajali tu...
Mwaka 1981 Thomas Sankara alikuwa
waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais wa wakati
huo wa Burkinabe ya zanani (Upper Volta) Jean Baptiste Major. Dr. na
baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi
Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali
ya Rais Major Jean Baptiste Dr kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi
kwa watu wote wa Volta ya Juu na kupendelea Marxist Revolution
theories..
Thomas Isidore Noël Sankara alikuwa Rais wa Upper
Volta (Volta ya Juu) kuanzia mwezi Agosti 4 1983 hadi mwezi Octoba 15
1987 baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Major Dr Jean Baptiste
yakiongozwa na Blaise Compaore na kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au
BURKINA FASO baada ya kubadilishwa jina na Sankara.
Thomas
Sankara aliyejulikana kama Che – Guevara wa Afrika alianzisha Program
mbalimbali za kijamii na kiuchumi kuleta mabadiliko katika nchi za
Afrika. Alibadilisha Upper Volta na kuwa Burkina Faso (land of Upright
Men).
Alianzisha kampeni ya kuboresha Elimu na kutanua
Huduma
za Afya kwa watu wa Burkina Faso maeneo ya vijijini hasa kwa watoto
walio athirika na magonjwa ya Uti wa mgongo , Homa ya manjano, na
surua.. na watoto karibu milioni 3 walipata tiba hizo..
Pia alianzisha kampeni ya upandaji wa miti kitaifa, na takribani miti Milioni kumi ilipandwa nchi nzima..
Pia alianzisha kampeni ya usafi nchini kote, kila mwananchi alipaswa
kufanya usafi eneo alipo.. na Sankara mwenyewe alikuwa anashika fagio na
kuingia barabarani kufanya usafi.. Hiyo ni kampeni iliyoitwa mfagio wa
mwananchi (le balai citoyen).
Aliongeza idadi ya wanawake katika
serikali yake, ikiwa ni kampeni yake nchi nzima kupinga tohara kwa
wanawake, pia alianzisha kampeni na baadae utaratibu wa kisheria wa
kuwataka wasichana waliopata mimba wakiwa mashuleni kuendelea na
masomo... pia akaajiri wanawake jeshini, akawapa ajira katika sekta za
umma.. ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuleta uwiano na usawa
nchini Burkina Fasso.
Pia ndoa za wasichana wadogo na za kulazimishwa haswa za kimila katika maeneo mengi ya Burkina Fasso zikapigwa marufuku..
Thomas Sankara ambaye hakutaka makuu kabisa na wananchi wa Burkina
Fasso. Akiwa kama Rais wa nchi, alivaa nguo zilizotengenezwa Burkina
Faso badala ya suti kutoka Paris na London.. mara nyingi alionekana
akiwa kwenye gwanda la jeshi..
Pia.. Thomas Sankara alifuta
matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi na watumishi wote wa umma,
yeye kama Rais alikuwa akitumia baiskeli au miguu kwenda kwa wananchi
vijijini kuhimiza na kusimamia shughuli za kimaendeleo..
Alijikita sana kwenye kusimamia na kukuza sekta ya afya katika
Burkinabe, alihimiza watu kujihusisha na kilimo.. akiwapelekea zana za
kilimo na pembejeo bure kwa watu wa vijijini na kugawa ardhi kwa
wananchi ili wajihusishe na kilimo..
Kwa muda mfupi sana akiwa
kama Rais wa Burikna Fasso, aliweza kuifanya nchi hiyo kuagiza chakula
kutoka nchi za nje na kuifanya nchi hiyo kuanza kuuza vyakula vyake
nje.. akaanza kuifanya Burkina Fasso kuwa imara kiuchumi.
Sankara aliwahimiza watawala wa Afrika waache kuwaibia wananchi, waache kutegemea sadaka kutoka nje.
Sankara akawaambia madeni ya Afrika hayana uhalali kwa vile yalitokana na mikataba mibovu.
Ndio maana hakuna maendeleo yaliyotokana na mikopo ya kigeni.
Sankara akataka Afrika iache kulipa madeni yasiyolipika.
Mwalimu Nyerere naye wakati huo alisema mtu hawezi kulipa madeni wakati watoto wanakufa njaa.
Thomas Sankara alisema ukitaka kujua maana ya ubeberu angalia sahani
yako ya chakula, utaona kila aina ya chakula unachokula kinatoka nje.
Ndipo akahimiza Afrika ijitegemee kwa chakula, akisema: "Anayekulisha
anakutawala"
Thomas Isidoré Nöel Sankara ni wazi aliwakasirisha
sana mabeberu wa kimagharibi, hasa ubeberu wa Kifaransa uliokuwa
ukitawala kupitia vibaraka wake wa Afrika kama Rais Felix Houphouet-
Boigny wa Ivory Coast...
Chini ya uongozi wake (Thomas Sankara), Burkina Faso ililima chakula chake badala ya kuagiza kutoka nje...
Kwa hatua hiyo, Thomas Sankara akawa amewaudhi wakubwa wa dunia
(mabeberu) kwa kukataa kwake mipango ya kurekebisha uchumi ya Benki ya
Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) huku hoja kubwa ya sankara
ikiwa ni kwamba, mipango hiyo ni ya kinyonyaji.
Thomas Sankara
aligawa ardhi kwa wakulima wadogo baada ya kuchukua kutoka kwa
wawekezaji wa nje ambao walikuwa wameipora baada ya kupewa na uongozi
uliopita..
Katika huduma za jamii alileta mabadiliko makubwa
katika huduma za elimu, afya, maji na kuboresha miundombinu ya barabara
kuunganisha sehemu mbalimbali za nchi hiyo.
Sankara katika
kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinahudumia wanachi wa kawaida,
Sankara alipambana na rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma,
huku akimtaka kila mwananchi kujituma kulijenga taifa.
Thomas
Sankara alikuwa mtu anayechukia rushwa na ufisadi, uvivu, uzembe,
dhuluma na unyonyaji wa wananchi na rasilimali zao. Alitaka kuona watu
wake wakifaidika kwa rasilimali za nchi yake.
Huyu ndiye Thomas
Sankara ambaye alipunguza mshahara wake hadi dola 450 kwa mwezi, ambaye
alitembea kwa baskeli katika mitaa ya Ouagadougu bila ya kulindwa.
Alipoulizwa kwanini hana walinzi alisema wananchi ndio walinzi wake,
hivyo hahitaji kuambatana na wanajeshi wenye bunduki.
Washauri wake mara kwa mara walimshawishi aachane na matumizi ya baisikeli.
Akaamua kutumia gari lenye bei ya chini (Renault 5) badala ya msururu wa mashangingi kama tuonavyo leo katika Afrika...
Hata hivyo alibaki na baiskeli yake mpaka alipokutwa na mauti, na
akaunti yake ya benki ilikutwa na akiba ya dola 400 ambayo ni sawa na
Tsh 850, 550/= (laki nane elfu hamsini na tano namia tano hamsini), kwa
sasa, badala ya mabilioni mengi kama wanayoficha huko Uswisi watawala
wetu leo...
Kumbuka, Thomas Sankara amedumu kwenye uongozi kwa
kipindi cha miaka 4 pekee kabla ya mapinduzi yaliyoongozwa na Rafiki
yake kipenzi... Blaise Compaore.. ambayo yaliondoka ba uhai wake, lakini
kwa kipindi hiko cha miaka 4 akihudumu kama Rais, alitengeneza mageuzi
makubwa sana..
Ndoto kubwa ya kila siku ya Thomas Sankara,
ilikuwa ni kuifanya Burkinafasso kuwa moja kati ya mataifa makubwa
Afrika kiuchumi..
Thomas Sankara alikataa hata picha yake (yeye
kama Rais) kutundikwa katika majengo, na taasisi za serikali.. alisema
hataki kutukuzwa..
Sankara alikuwa akipokea mshahara wa dola 450 kwa mwezi, mshahara mdogo kuliko viongozi wote barani Afrika kwa wakati huo..
Huyu ndiye Thomas Isidore Noël Sankara anayejulikana kama Ernesto Che
Guevara wa bara la Afrika (alikuwa akivaa mavazi kama Che Guevara,
mwenendo, matendo na malengo yake yalifanana na Ernesto Che Guevara, pia
walikuwa marafiki wakubwa).., aliyeiongoza nchi kwa muda wa miaka minne
kabla ya kuuliwa na maadui wa mapinduzi wakiongozwa na kapteni Blaise
Compaoré Aliuliwa nyakati za usiku na mara moja akazikwa kwa haraka.
Ernesto Che Guevara naye alikuwa mwanamapinduzi wa Marekani Kusini
aliyeuliwa na majasusi wa Marekani (CIA) na kisha kuzikwa kisirisiri.
Thomas Sankara aliyekuwa muumini wa fikra za kupigania Umoja wa Afrika
au Pan Africanist mara nyingi alionekana kutopendwa na mataifa ya
magharibi kutokana na fikra zake za kupinga dhuluma za wakoloni kunyonya
watu wanyonge.
Mwaka 1985, Thomas Sankara alikaririwa akisema kuhusu falsafa yake kisiasa iliyokuwa maarufu, ilikuwa ikisema;
‘you cannot carry out fundamental change without a certain amount of
madness’, yaani kwa tafsiri isiyo rasmi, hauwezi kuleta mageuzi ya
msingi bila kuwa na kiasi fulani cha ukichaa... ndiyo maana mabeberu
walieneza propaganda kwamba Sankara ni kichaa anayeingoza Burkina
Fasso..
Pamoja na yote na mengi mazuri.., wapinzani ndani na nje
ya nchi ya Burkinafasso, walisikika wakimlaumu Sankara kwa kupiga
marufuku vyama huru vya wafanyakazi na vyama vya siasa.
Pia
Sankara alianzisha Mahakama za wananchi ‘people’s revoluntionary
tribunals’ ambazo zililenga kutoa hukumu kwa wapinga mapinduzi,
wafanyakazi wazembe... Jambo ambalo lilileta hamasa ya watumishi wa umma
kufanya kazi kwa nguvu wakiogopa hukumu..
Ila hatua hiyo ilipigwa vita saba na wapinzani wake..
Kumbukumbu kubwa ya wananchi wa Burkinabe (Burkina fasso), kuhusu
Kapteni Thomas Sankara, ilikuwa ni wiki moja kabla ya kuuwawa kwake
alitabiri, na alikaririwa akisema:
“Wanamapinduzi wanaweza kuuliwa, lakini fikra za kimapinduzi zitaendelea kuishi daima”
Hapo alikuwa akinukuu maneno ya Mwanamapinduzi maarufu Duniani, Ernesto Che Guevara ambaye aliwahi kusema..
“Revolutionaries and individuals can be murdered, but ideas never die.”
Thomas Sankara alifariki Oktoba 15 mwaka 1987 baada ya kupinduliwa na
Blaise Compaore kuchukuwa utawala nchini Burkina Faso kwa muda wa miaka
27..
Inafahamika kwamba, kwa mara ya kwanza mwaka 1997, familia
ya marehemu Thomas Isodoré Noël Sankara, ilifikisha ombi la kutaka mwili
wa Sankara ufukuliwe ili ufanyiwe uchunguzi..
Taarifa
zinafahamisha kuwa serikali ya Blaise Compaore ilitupilia mbali ombi
kutoka familia ya Thomas Sankara la kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu
kifo cha Sankara.
Kwa mujibu ya ripoti ya kifo cha Thomas Sankara, serikali ilifahamaisha kuwa Thomas Sankara alifariki kifo cha kawaida.
Familia ilitaka kufahamu kama ni kweli katika kaburi hilo ndipo mwili wa Thomas Sankara ulipohifadhiwa..
Blaise Compaoré ni nani??
Compaoré alizaliwa katika mji wa Ziniaré, uliopo umbali wa kilomita 43
kutoka Jiji la Ouagadougou, ambao ndiyo mji mkuu wa Burkina Faso,
alipitia mafunzo ya kijeshi akiwa amefikia cheo cha kapteni.
Ni
mwanzilishi wa chama chake cha Congress for Democracy and Progress,
akihusika katika mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1983 na yale ya mwaka
1987. Miaka mitatu baada ya kufanya mapinduzi na kuingia Ikulu,
alichaguliwa rasmi Rais wa Burkina Faso kwa kura mwaka 1991, katika
uchaguzi uliosusiwa na upinzani na kisha alichaguliwa tena kwa njia hiyo
ya kura katika chaguzi za mwaka 1998, 2005 na 2010.
Alikuwa
gwiji wa kushiriki mapinduzi ya kung’oa na kupachika watu madarakani na
katika kuthibitisha hilo, akiwa na umri wa miaka 33, Blaise Compaoré
aliratibu mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Meja
Jean-Baptiste Ouedraogo nchini Liberia, hiyo ilikuwa Agosti 4 mwaka
1983. Wakati huo Burkina Faso ilikuwa ikiitwa Upper Volta.
Mapinduzi hayo ya kijeshi yaliungwa mkono na Libya chini ya Muammar
Gaddafi rafiki wa Compaore, kwa wakati huo, Libya ikiwa katika msuguano
na Ufaransa kuhusu Chad.
Washirika wengine wa mapinduzi hayo ya
Agosti 4, mwaka 1983 ni Kapteni Henri Zongo, Meja Jean-Baptiste Boukary
Lingani na Kapteni Thomas Sankara— aliyetangazwa Rais kuwa katika
mapinduzi hayo ya kijeshi.
Compaoré wakati huo alipofanya tena
mapinduzi ya kijeshi mwaka 1987, alizungumzia mauaji ya rafiki yake wa
jeshini zamani (Rais Sankara) ambaye alimsaidia kuingia Ikulu (mwaka
1983) akisema ilikuwa ajali tu.
Hata hivyo licha ya kuongoza
mapinduzi ambayo si tu yalimng’oa rafiki yake huyo madarakani bali hata
kumuua, licha ya kukaa kwake Ikulu kwa miaka 27, Compaore hakuwahi
kuchunguza sababu za mauaji hayo ya Sankara, jambo linalozua hisia
kwamba alishiriki kuhakikisha Sankara anauawa ili mapinduzi yatimie bila
Katika utawala wa rafiki yake (Sankara), ulioanza mwaka 1983 hadi mwaka
1987, Compaoré aliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, akiwa
amepata kutumikia cheo cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Naibu Waziri
wa Sheria..
BLAISE Compaoré aliyeitawala Burkina Faso kwa muda
wa miaka 27 alilazimishwa na wananchi kuikimbia nchi hiyo tarehe
31-10-2014.. Amekimbilia Ivory Coast (Cote d’Ivoire) ambako anahifadhiwa
na rafiki yake Rais Alassane Ouattara...
Hii ni baada ya wananchi wenye hasira walipojitokeza kwa maelfu mitaani katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Tatizo lilianza pale Blaise Compaoré alipotaka kubadili Katiba ili
aendelee kutawala. Bunge lilikuwa tayari kutii amri yake. Ndipo wananchi
wakalichoma moto jengo la Bunge na ofisi za serikali pamoja na makao
makuu ya chama tawala cha CDP (Congress of Democracy and Progress).
Baadhi ya nyumba za wabunge waliokuwa mstari wa mbele katika kutetea
Compaoré aongezewe muda nazo zilichomwa moto.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Burkina Fasso Honoré Traore akajitangaza kuwa Rais mpya. Wananchi wakamkataa.
Baada ya muda Honoré Traore akapigwa kikumbo na Luteni Kanali Isaac
Yacouba Zida akashika madaraka. Wananchi wakaendelea kudai serikali
watakayoichagua wenyewe kidemokrasia, wakisema hawakumfurusha Blaise
Compaoré ili jeshi lishike hatamu...
Wimbo mkubwa wa wananchi wa
Burkinabe ni kwamba... Blaise Compaoré alimuua kipenzi chao.. na hivyo
kusaliti mapinduzi ya haki ya awali yaliyoongozwa na Thomas Sankara
dhidi ya serikali ya Jean Baptiste Ouedraogo.
Vyombo vya
propaganda chini ya serikali ya Blaise Compaore wa kwamba Thomas sankara
hakuwa muhimu sana katika uwepo wa taifa hilo,...
Hata mapinduzi
ya wananchi wa Burkina Fasso dhidi ya Compare walihamasishwa na
kumbukumbu za Kapteni Thomas Sankara. Ingawa watawala wanajaribu kufuta
kumbukumbu zake lakini wananchi wa kawaida wangali wanamkumbuka.
Ni vizuri ikumbukwe kuwa hii ni mara ya tisa kwa majeshi kuvamia urais
wa Burkina Faso tangu nchi hiyo kupata uhuru wa bendera kutoka Ufaransa
mwaka 1960. Ni uhuru wa bendera kwa vile leo nchi hiyo inaendelea
kukaliwa na majeshi ya Ufaransa, na utajiri unaporwa na wawekezaji.
Kwa sababu hata mapinduzi ya Blaise Compaore kumuondoa rafiki yake
Thomas Sankara yaliongozwa na Compaore akisaidiwa na Ivory Coast,
ufaransa na wakafanikiwa kumuua Sankara..
Wanamapinduzi na wana
mageuzi wote Duniani, ni watu wanaojulikana kama wapinga ubeberu
waziwazi na ndiyo maana wengi wao wamekumbana na ukatili wa mabeberu.
Wako wana mapinduzi na wana mageuzi waliouawa kama akina Thomas Sankara
wa Burkina Fasso na Patrice Lumumba wa DR Congo na wengine kutumikia
vifungo virefu na vya maisha maisha kama Nelson Mandela.
(Makala hii imeandikwa kwa msaada mkubwa wa mashirika mbalimbali ya habari ya kimataifa)
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment