Uongo wa Historia ya Afrika na Waafrika itajibiwa na muafrika.
Binafsi nimejipa utaratibu kuwa vitabu vinavyohusu uafrika na waafri
sitavitilia mkazo sana vile vilivyoandikwa na wazungu bali
vilivyoandikwa na Waafrika wenyewe! Mfano ukisoma historia ya Mkwawa
iliyoandikwa na wazungu wanasema mkwawa alijiua kwakujipiga risasi,
Ukweli wa historia ya kiafrika wazungu waliona aibu kusema walimshindwa
Mkwawa, Mkwawa hakujiua bali aliwatoroka wazungu na kuelekea Songea
ambapo alifia milima ya Lukumbulu kwakuliwa na Simba baada ya kuugua
akiwa milimani peke yake. Nimpongeze kamanda Edwin Mwesiga huyu ni
mtafiti wa mambo ya kiafrika na uafrika wetu.
Ni rahisi sana
Vijana wa leo kuwadhalau wazee wanaokutana nao barabarani na kuwaona
watu wasio na Elimu wakiaminishwa kuwa elimu ilianzia magharibi, Cha
ajabu Ahmed Baba (1556-1627) karne ya 16 aliandika vitabu 60.Ni mingoni
mwa wasomi wa Phd katika ufalme wa Mali.
Ni vizuri watu tuyasake
maarifa kwakutumia maarifa, na kwakutokujua historia yetu Waafrika
tumelidhika Bara letu la Afrika na yale machache tunayoyafahmu,
tukidhani wazungu ndio wasomi wa mwanzo duniani kumbe wapo waliofanya
mapinduzi makubwa katika Africa,ila wamefichwa na historia za kigeni
zinazofundishwa mashuleni.
Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni
aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo
mkubwa......Pamoja na kwamba 1927 Gavana Sir David Cameron kupiga
marufuku mtu mweusi kukanyaga mjini (posta ya leo) hasa kwenye sherehe
za wazungu ambazo zilikuwa maranyingi zinafanyikia ukumbi wao pale makao
makuu ya NBC leo,
Gavana huyu aliwaundia chama cha kuratibu
sherehe za weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba)
na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia
ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil
Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la
Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu mateka wa vita vya
kwanza vya dunia toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo
na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).
Hao ndio mwaka 1927
waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi
Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu.
(Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola
alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana
Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na
mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwakil Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana
vita vya pili vya dunia, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka
vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani. Kisha AA
ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto
Kyaruzi (Mhaya)huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa
kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwakil Sykes na Mweka hazina
akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi
ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo
Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU
iliyokwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM
ambacho kinalitafuna taifa leo..
Hili ndio chimbuko la AA, TAA, TANU na hii CCM.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment