Kumekuwa na maneno yanasemwa na mimi kupuuza katika kipindi cha wiki
kadhaa; kwamba ninapanga kumhujumu Rais Magufuli katika kazi zake.
Maneno haya yanaenezwa na watu wanaotumwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Bwana Charles Kitwanga ( nina ushahidi usio na mashaka wa Kitwanga
kupanga vijana wa wanaojiita wa UVCCM kufanya mikutano na waandishi wa
habari na anawalipa fedha kufanya hivyo. Nataka ifahamike bila chenga
kama ifuatavyo:
1) Ninamwunga mkono Rais katika kazi ya kusafisha
Nchi. Hii ndio kazi nilikuwa nafanya katika kipindi cha miaka 10
iliyopita. Nitakuwa mtu wa ajabu sana nisipomwunga mkono Rais katika
vita dhidi ya Ufisadi. Hata hivyo, kamwe sitasita kuweka wazi pale
ninapoona Rais anafanya makosa. Na nimekuwa nikisema wazi wazi na
kumkosoa Rais waziwazi. Lakini pia nimekuwa nikimwambia Rais kwa njia
nyengine ambazo viongozi huwasiliana ninapoona anafanya sivyo. Kukosoa
ni kazi moja muhimu sana na ya kizalendo kuliko lolote ambalo raia
anaweza kufanya kwa kiongozi wake. Kukosoa Serikali ni uzalendo
maradufu. Pale panapostahili nitapongeza.
2) Namsihi Waziri
Kitwanga amalize matatizo yake yeye mwenyewe. Yeye kama mmiliki wa
Kampuni ya Infosys yenye mkataba na Serikali katika Wizara anayoongoza
sasa anapaswa aone ni namna gani hana mgongano wa maslahi. Waziri
Kitwanga asitafute watu wa kuwatupia lawama kwenye mambo yanayomhusu.
Mimi binafsi sijawahi kugombana na Charles Kitwanga. Hajawahi kuwa
rafiki yangu. Hajawahi kuni excite kama Kiongozi ( kimsingi nashangaa
mtu kama yeye kuweza hata kuwa Waziri wa Wizara nyeti kama hiyo) . Zaidi
ya yote Waziri Kitwanga sio 'size yangu'. Kwa protokali za Uongozi,
size yangu mimi ni Rais Magufuli, bosi wake. Naanzaje kuhangaika na
Kitwanga? Ili iweje? Namsihi asijipandishe chati kwamba mimi nataka
kumtoa. Ningetaka kumtoa wala asingejua maana ningeshughulika na
aliyemteua. Nasema haya sababu amekaa na Waziri Mkuu na Wabunge kadhaa
akilalamika kuwa nataka kumtoa Uwaziri. Asinipe dhambi, Uwaziri
atatolewa na aliyemteua kwa madhambi aliyofanya. Asitafute bangusilo!
3) Mimi kwa wiki kadhaa sasa nipo nje ya Nchi ( nchini Marekani katika
Chuo Harvard kwa masomo) . Sijui na sihusiki na njama zozote dhidi ya
yeyote. Kwanza hizo sio aina ya siasa ninazofanya. Siasa ninazofanya ni
Siasa za Maendeleo ya Wananchi na sio Siasa za kuwinda watu.
4)
licha ya kuwa Kiongozi wa Chama, Mimi ni Mbunge wa Chama Cha ACT
Wazalendo. Kwa hiyo nafuata maelekezo ya chama changu katika kazi zangu.
Chama changu katika Mpango Mkakati wake kimeniagiza kufanya Siasa za
Maendeleo. Chama changu kinaunga mkono juhudi zote za Rais kurejesha
imani ya wananchi kwa Serikali kwa kupambana na ufisadi. Hata hivyo
Chama Cha ACT Wazalendo kinamtaka Rais ajenge mfumo imara wa kitaasisi
ili mapambano dhidi ya ufisadi yawe endelevu. Hivyo, porojo za kwamba
nataka kumwangusha Rais ni porojo za watu wasionijua binafsi na wasiojua
misingi ya ACT Wazalendo
5) Nawasihi Watanzania wote a) kumdharau
Waziri Kitwanga na kumtaka ajibu tuhuma zinazomkabili za Kampuni yake
binafsi kufanya kazi na Idara katika Wizara anayosimamia na kwamba
ajipime kama anatosha kuendelea kumsaidia Rais kazi b) kuendelea
kumwunga mkono Rais katika vita dhidi ya ufisadi. Kama nilivyosoma mwaka
jana ' asiyemwunga mkono Magufuli yupo upande wa mafisadi' c) kuepuka
siasa za porojo zinazoendeshwa na vijana wanaotafuta nafasi za kuteuliwa
na d) kutaka umadhubuti wa kila jambo linasomewa ili kuepuka kuonea
watu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment