Ernest Jumbe Mangu
Utumishi: 2013 - 1970 (Mkuu wa Jeshi la Polisi) Taarifa za Kina Tarehe ya Kuzaliwa: 1959 Mahali pa Kuzaliwa: Singida Ndoa: Ameoa |
Ernest Jumbe Mangu alizaliwa mwaka 1959 mkoani Singida. Alipata elimu ya Sekondari katika Shule ya Tumaini mwaka 1981.
Alijiunga na Jeshi la Polisi kwa mafunzo ya awali katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) Agosti 17 mwaka 1982 na kuhitimu mafunzo yake mwezi Juni mwaka 1983. Mwaka 1987 alipata mafunzo ya sheria kwa ngazi ya cheti katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwezi Novemba mwaka 1992 alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Mwezi Juni mwaka 2010, alitunukiwa shahada ya udhamili katika masuala ya usalama katika Chuo Kikuu Cha Usalama cha Marekani.
Akiwa ndani ya Jeshi la Polisi amepandishwa vyeo mbalimbali vikiwemo Koplo wa Polisi (1988), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1992), Mkaguzi wa Polisi (1995), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (1997), Mrakibu wa Polisi (2002), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2004), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2006), Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (2010), Naibu Kamishna wa Polisi (2013) na Kamishna wa Polisi (2013).
Amewahi kufanya kazi kama Mkuu wa
Upelelezi Mkoa wa Mwanza, Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Pwani na
Mwanza na Kamishna wa Intelijensia ya Jinai.
Omari I Mahita
Utumishi: 1996 - 2006 (Mkuu wa Jeshi la Polisi .) Taarifa za Kina Tarehe ya Kuzaliwa: - Mahali pa Kuzaliwa: Morogoro, Tanzania Ndoa: Ameoa |
Said Ally Mwema Utumishi: 2006 - 2013 (Mkuu wa Jeshi la Polisi) Taarifa za Kina Tarehe ya Kuzaliwa: - Mahali pa Kuzaliwa: Kilimanjaro, Tanzania Ndoa: Ameoa |
0 comments:
Post a Comment