mwanazuoni

MEYA WA DAR ES SALAAM - NILITEMBEA PEKU KWENDA SHULE MIAKA SABA

  • Baraza la Madiwani kuwa wazi kwa wananchi
  • Asema yeye ni Simba Damu
MWEZI uliopita, Isaya Charles Mwita, alichaguliwa na madiwani wenzake kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam,; akiweka historia ya kuwa meya wa kwanza kutoka chama cha upinzani kwenye jiji hilo.
Raia Mwema limefanya naye mahojiano wiki hii ambapo ameeleza kuhusu historia yake na ndoto zake katika wadhifa wake huo mpya. Endelea.
RAIA MWEMA: Ni mara yako ya kwanza kufanya mahojiano na chombo cha habari cha kitaifa, Raia Mwema, ni vyema ukaeleza kwa ufupi historia yako kabla ya kutwaa nafasi hii ya umeya.
ISAYA: Nimezaliwa Wilaya ya Tarime, nimekulia kule nikiwa katika familia ya watoto sita, tukiwa na dada yetu mmoja.Tumboni mwa mama yangu nilikuwa mtoto wa nne.
Katika maisha yetu, baba yetu alituacha tukiwa wadogo sana miaka ya 1976 huko nyuma. Kwa hiyo tukabaki na mama yangu mzazi, yeye ndiye aliendelea kutulea watoto sita wale, ilikuwa ni shida sana.
K usoma kwetu ilikuwa ni shida kwa sababu nakumbuka mama yangu wakati anatulea alikuwa anauza kuni, mkaa ili watoto wake tuweze kusoma. Alifanya hivyo kwa mapenzi makubwa kama wazazi wengine wa kiafrika wanaohangika kulea wakati unapokuwa umefiwa na mume.
Akatusukuma na siku zote mama alituambia elimu ndiyo itakayotuokoa. Kwa hiyo mimi kwa nafasi yangu nikaendelea kujisukuma na kusema kweli niliipenda shule japo umasikini ulikuwa ni sehemu ya maisha yangu.
Nakumbuka nilisoma darasa la kwanza mpaka la saba sikuwahi kuvaa viatu. Nilitembea peku, maisha yalikuwa magumu sana. Hata nilivyomaliza masomo yangu ya msingi sikubahatika kufaulu, kwa hiyo ilinilazimu nirudie darasa tena mpaka hapo nilipopata nafasi ya kufaulu ya kuendelea na kidato cha kwanza.
Lakini huko kote nilikokwenda hali ilikuwa ngumu, ada nilikosa ilinilazimu nifanye vibarua vya kulima kwa walimu wangu wa sekondari ili niweze kujikimu kimaisha, lakini maisha yaliendelea mpaka leo.
Lakini kipindi chote cha masomo yangu hadi kidato cha tano na sita nilipambana na maisha, napikia watoto nyumbani, maana dada yangu aliolewa na mama yangu aliugua miguu kwa miaka minne.
Kwa hiyo kipindi chote cha kusoma kwangu nililima ili niweze kujilipia ada huku nikijua kwamba siku moja nitafaulu, sikuwahi kukata tamaa. Pamoja na kufaulu kuingia kidato cha tano, nako hali ilikuwa ngumu kuweza kulipa ada.
Nikachukuliwa na binamu yangu akaanza kunifundisha shughuli ndogondogo za biashara ambazo zilinisaidia kupata fedha na kuendelea na elimu yangu ya kidato cha tano. Baada ya kumaliza elimu yangu ya kidato cha sita nilibahatika kuendelea na elimu ya Chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini nikichukua fani ya uchumi.
Baada ya kumaliza elimu yangu pale chuoni, nilibahatika kuisaidia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa utaratibu wa kujitolea kama mchumi, na mwisho nikaamua kufanya shughuli zangu binafsi huku nikijishughulisha na siasa.
Hayo maisha yalinipelekea mimi kuchukia kabisa mfumo wa kiserikali, nikajikuta napenda upinzani kwa sababu nikaona upinzani ndiyo tunaofanana.
Niliona jirani zangu watoto wao wakisoma shule binafsi, maisha yao mazuri, wanakula vizuri wakati wengine nikiwamo mimi, tukiwa na maisha magumu. Hali hiyo ilinifanya nikachukia sana mfumo wa maisha wa namna hiyo.RAIA MWEMA: Uamuzi wa kuwania nafasi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam ulikuwa ni wako binafsi au chama chako cha Chadema kilikutaka ufanye hivyo?
ISAYA: Ulikuwa ni uamuzi wangu mwenyewe. Nilitaka kuwania udiwani ili nije kugombea nafasi ya umeya, kabla hata sijawa meya baadhi ya wanachama wetu walishaanza kuniita Meya.
Hata mratibu wangu wa chama alikuwa akiniita Meya hata kabla sijatangaza kuwania nafasi hiyo. Nakumbuka hata wakati wa kampeni mwaka 2015, aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji, alikuja Kigamboni kufanya kampeni na sikutambulishwa kama mwenyekiti wa Chadema Kigamboni bali nilitambulishwa kama Meya mtarajiwa kama vile watu walikuwa wakiotea maisha yangu ya baadaye.
RAIA MWEMA: Kabla hujawa Meya, ni mambo gani ulikuwa ukitamani yabadilike hapa Dar es Salaam?
ISAYA: Kama nilivyotangulia kusimulia juu ya maisha yangu, siridhishwi na huduma zilizokuwa zikitolewa na serikali, hasa huduma za jamii. Suala la shule, hususani kipindi ambacho kwa Dar es Salaam watoto wengi shuleni kote wanakaa chini. Unaenda shuleni, kwa bahati mbaya shule nzima ina watoto 400, darasa moja lina watoto 250. Nilikuwa nikifika pale nilirejea maisha niliyopitia, ilikuwa inaniuma sana, nikawa natamani wananchi wanisaidie mimi kuwa diwani ili niwasaidie.
Niwasaidie si kwa kutafuta fedha ya serikali bali ningechangisha Watanzania wenzangu kuwahamasisha ili angalau tuweze kununua madawati. Naomba nikwambie jambo moja ambalo wengi hawalifahamu kwamba baada tu ya kuchaguliwa nilijenga madarasa saba kwa mwezi mmoja huko katika kata yangu ya Vijibweni, Kigamboni.
Nilifanya hivi baada ya kuwahamasisha wananchi kuchangia kwa kushirikiana na kampuni mbalimbali. Maadam nimekuwa Meya, sitaki kusikia vilio vya madarasa na madawati katika jiji hili.
RAIA MWEMA: Kwa nafasi yako ya Umeya, unadhani ni changamoto gani kubwa inayokabili jiji na namna unavyofikiria kupata utatuzi wake?
ISAYA: Changamoto ambayo naiona ni huduma za jamii ambazo nimetangulia kuzisema kwa upande wa elimu na afya. Kwa mfano, unaweza kwenda hospitalini unakuta mama amelala chini baada ya kujifungua.
Jambo hili linashindwa kabisa kuniingia akilini kwa sababu jiji hili lina vyanzo vingi vya mapato. Naomba kutumia nafasi hii kuwaomba wahisani wa ndani na benki zetu kujitolea kutusaidia.
Dar es Salaam ni mji maarufu na muhimu hapa nchini. Tunazo benki, hawa wanaosimamia benki hizi wengi wao wamesoma maisha ya shida kweli lakini wamefika sehemu wamejisahau. Yaani nchi hii imefika mahali ambapo hakuna mtu anayejali mtoto wako kukaa chini. Hakuna mwenye kutaka kujua kwa sababu watoto wao wote wamewapeleka katika shule za kimataifa.
 RAIA MWEMA: Najua una mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu. Katika mwaka huu wa 2016, ni mambo yapi unadhani utakuwa umeyatekeleza kufikia mwisho wa mwaka?
ISAYA: Kwanza ninapata wakati mgumu sana kuahidi kwa sababu sijaitisha bado kikao cha Baraza la Madiwani. Unajua unaahidi kile ambacho kimeshapitishwa na baraza hilo. Sasa hivi naweza kuahidi kitu na baadaye baraza likaja kunigomea kwa sababu ule ni mjadala unaendeshwa.
Nadhani tutakuwa na mjadala mzuri ndani ya Baraza la Madiwani na pale tutakubaliana kuhusu kipaumbele. Kipi kitaanza na yapi yatafuata.
Kwa hiyo tutakapokutana tutakubaliana utekelezaji wa vipaumbele vyetu. Nadhani siku zijazo, pengine baada ya Aprili 18 wakati madiwani wote watakapokutana, tutakuwa tumeshapata kitu cha kuwaambia na namna ya utekelezaji wake.
RAIA MWEMA: Una maoni gani kuhusu mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (DART) na namna gani utasaidia kuhakikisha huduma hii inanza haraka iwezekanavyo?
ISAYA: Kama unavyofahamu nina siku ya tatu tangu niingie ofisini (Aprili 1, 2016), hivyo sijapata ripoti yoyote, tutakapokaa pamoja na menejimeti watanipa taarifa.
RAIA MWEMA: Dar es Salaam inakabiliwa na kero ya maji kwa upande wa baadhi ya maeneo, ikiwemo Ubungo, Kimara, Mbagala na maeneo mengine pembezoni mwa jiji. Ni namna namna gani umejipanga kumaliza changamoto kwa wananchi wa Dar es Salaam?
ISAYA: Kwanza lazima tukubali kwamba kuna miradi ambayo inaendelea. Nimepata taarifa kwamba mradi wa Ruvu Juu sasa hivi uko vizuri, mradi wa Kwembe pia unakwenda vizuri.
Inawezekana mwaka huu kwa mujibu wa maelezo ya mainjinia, maji yanaweza kupatikana kwa Jimbo la Kibamba, Ubungo, Kawe na Segerea.
Lakini kuna watu ambao huu mradi unawaacha kwa mfano watu wa Mbagala na Kigamboni lakini nafahamu kwamba kuna mradi wa maji wa Kimbiji ambao maeneo haya ndiyo yanauhusu. Lakini kwa kuwa wamenichagua mimi Isaya Mwita kuwa meya wao, basi mradi wa Kimbiji utatekelezeka.
 RAIA MWEMA: Kulikuwa na figisufigisu nyingi wakati wa mchakato wa kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Utafanya nini kuhakikisha kunakuwa na mshikamano katika baraza litakalokuwa likikutana?
ISAYA: Nimeshasema na ninarudia kusema kwamba mimi au sisi tumekwishafika hapa, tunataka tufanye kazi. Watanzania wanataka maendeleo, nasi Ukawa tumepewa miaka mitano na baada ya miaka mitano hii na CCM hao unaowaona watasimama na kusema kwamba, tuliwaambia kwamba hawa watu hawafai, tungewapa nchi ingekuwaje?
Tumewapa Dar es Salaam, wamefanya nini? Kwa hiyo ninapaswa kutoa matokeo chanya, nataka nifanye kazi naomba mlipe kodi.
Nawaambia wana Dar es Salaam, kwa yule anayepaswa kulipa kodi ya majengo, na kodi nyingine mbalimbali lazima walipe.
Tumesema tutakuwa tunawatangazia kila makusanyo na namna yalivyotumika. Na baraza langu naomba niwaambie waandishi wa habari litakuwa linatangazwa. Hata tunaloliandaa litatangazwa kwenye vyombo vya habari. Mje mshuhudie, ni utaratibu mpya, na ndivyo kanuni inavyotaka. Ningekuwa na uwezo ningerusha moja kwa moja kupitia televisheni na redio nchini.
RAIA MWEMA: Kipindi mnajiandaa kuchagua Meya kulikuwa na tetesi kwamba sakata la UDA ilikuwa ni kikwazo kwa Ukawa kupewa jiji. Kwamba chama tawala hakikuwa kinataka mpate fursa ya kuibua yale yasiyopaswa kujulikana. Je, ni namna gani mmepanga kushughulikia suala la UDA?
ISAYA: Faili la UDA nimeletewa na tayari liko hapa mezani kwangu, naanza kulisoma leo. Sasa niseme nini tena hapo? Nimepanga kwamba nitasoma kila ukurasa kwa umakini wa hali ya juu. Tutasaidiana na wanasheria wa ndani na wa nje kama kutakuwa kuna lazima ya kufanya hivyo ili Watanzania wajue shirika lao likoje. Lakini pia naamini haki itatendeka.
RAIA MWEMA: Nje ya siasa unapenda mambo gani?
ISAYA: Nje ya siasa, kwanza nampenda Mungu sana. Lakini mbali na hapo pia napenda mpira unaochezwa nje ya nchi na ndani pia. Mimi ikifungwa timu ya Simba huwa napata machungu sana lakini sina namna ya kufanya.
RAIA MWEMA: Dar es Salaam ni moja ya maeneo ya hapa nchini yaliyokithiri kwa uingiaji wa dawa za kulevya pamoja na matumizi yake. Umejipanga vipi angalau kupunguza kasi ya uingiaji kama si kumaliza kabisa?
ISAYA: Hili suala naamini vyombo vya usalama vinashughulikia. Tuna idara ya usalama wa taifa, wao hawa wana wajibu kwa sababu kimsingi wanawajibika kwa Rais wa chi, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria.
RAIA MWEMA: Unawaambia nini wananchi wa Dar es Salaam ambao wamewekeza matumaini kwako ili kuhakikisha jiji hili linakuwa mahala salama pa kuishi?
ISAYA: Wana Dar es Salaam naomba niwaombe sana, wanisaidie kulipa kodi. Tunaandaa utaratibu ambao utawezesha wao kulipa kodi, wasijisikie wanyonge, walipe, fedha zao tutazitumia vizuri.
Tukiweza kukusanya fedha vizuri tutaweza kufanya mambo yatakawapa usalama wa kiafya, kiuchumi, kijamii na kimiundombinu.
Ili wawe salama barabarani, ni lazima barabara ziwe nzuri. Hilo linahitaji fedha. Ili wawe salama kiafya, inabidi wakae sehemu zilizo salama na huduma za hospitalini na kwenye vituo vya afya ziboreshwe. Hilo linahitaji fedha.
Fedha hiyo itapatikana kutoka kwa wananchi wenyewe kupitia kodi zao.
Chanzo: Raia Mwema

usoma kwetu ilikuwa ni shida kwa sababu nakumbuka mama yangu wakati anatulea alikuwa anauza kuni, mkaa ili watoto wake tuweze kusoma. Alifanya hivyo kwa mapenzi makubwa kama wazazi wengine wa kiafrika wanaohangika kulea wakati unapokuwa umefiwa na mume.
Akatusukuma na siku zote mama alituambia elimu ndiyo itakayotuokoa. Kwa hiyo mimi kwa nafasi yangu nikaendelea kujisukuma na kusema kweli niliipenda shule japo umasikini ulikuwa ni sehemu ya maisha yangu.
Nakumbuka nilisoma darasa la kwanza mpaka la saba sikuwahi kuvaa viatu. Nilitembea peku, maisha yalikuwa magumu sana. Hata nilivyomaliza masomo yangu ya msingi sikubahatika kufaulu, kwa hiyo ilinilazimu nirudie darasa tena mpaka hapo nilipopata nafasi ya kufaulu ya kuendelea na kidato cha kwanza.
Lakini huko kote nilikokwenda hali ilikuwa ngumu, ada nilikosa ilinilazimu nifanye vibarua vya kulima kwa walimu wangu wa sekondari ili niweze kujikimu kimaisha, lakini maisha yaliendelea mpaka leo.
Lakini kipindi chote cha masomo yangu hadi kidato cha tano na sita nilipambana na maisha, napikia watoto nyumbani, maana dada yangu aliolewa na mama yangu aliugua miguu kwa miaka minne.
Kwa hiyo kipindi chote cha kusoma kwangu nililima ili niweze kujilipia ada huku nikijua kwamba siku moja nitafaulu, sikuwahi kukata tamaa. Pamoja na kufaulu kuingia kidato cha tano, nako hali ilikuwa ngumu kuweza kulipa ada.
Nikachukuliwa na binamu yangu akaanza kunifundisha shughuli ndogondogo za biashara ambazo zilinisaidia kupata fedha na kuendelea na elimu yangu ya kidato cha tano. Baada ya kumaliza elimu yangu ya kidato cha sita nilibahatika kuendelea na elimu ya Chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini nikichukua fani ya uchumi.
Baada ya kumaliza elimu yangu pale chuoni, nilibahatika kuisaidia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa utaratibu wa kujitolea kama mchumi, na mwisho nikaamua kufanya shughuli zangu binafsi huku nikijishughulisha na siasa.
Hayo maisha yalinipelekea mimi kuchukia kabisa mfumo wa kiserikali, nikajikuta napenda upinzani kwa sababu nikaona upinzani ndiyo tunaofanana.
Niliona jirani zangu watoto wao wakisoma shule binafsi, maisha yao mazuri, wanakula vizuri wakati wengine nikiwamo mimi, tukiwa na maisha magumu. Hali hiyo ilinifanya nikachukia sana mfumo wa maisha wa namna hiyo. - See more at: http://www.raiamwema.co.tz/meya-wa-dar-nilitembea-peku-kwenda-shule-miaka-saba-1#sthash.B8M0qjFA.dpuf
  • Baraza la Madiwani kuwa wazi kwa wananchi
  • Asema yeye ni Simba Damu
MWEZI uliopita, Isaya Charles Mwita, alichaguliwa na madiwani wenzake kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam,; akiweka historia ya kuwa meya wa kwanza kutoka chama cha upinzani kwenye jiji hilo.
Raia Mwema limefanya naye mahojiano wiki hii ambapo ameeleza kuhusu historia yake na ndoto zake katika wadhifa wake huo mpya. Endelea.
RAIA MWEMA: Ni mara yako ya kwanza kufanya mahojiano na chombo cha habari cha kitaifa, Raia Mwema, ni vyema ukaeleza kwa ufupi historia yako kabla ya kutwaa nafasi hii ya umeya.
ISAYA: Nimezaliwa Wilaya ya Tarime, nimekulia kule nikiwa katika familia ya watoto sita, tukiwa na dada yetu mmoja.Tumboni mwa mama yangu nilikuwa mtoto wa nne.
Katika maisha yetu, baba yetu alituacha tukiwa wadogo sana miaka ya 1976 huko nyuma. Kwa hiyo tukabaki na mama yangu mzazi, yeye ndiye aliendelea kutulea watoto sita wale, ilikuwa ni shida sana.
Kusoma kwetu ilikuwa ni shida kwa sababu nakumbuka mama yangu wakati anatulea alikuwa anauza kuni, mkaa ili watoto wake tuweze kusoma. Alifanya hivyo kwa mapenzi makubwa kama wazazi wengine wa kiafrika wanaohangika kulea wakati unapokuwa umefiwa na mume.
Akatusukuma na siku zote mama alituambia elimu ndiyo itakayotuokoa. Kwa hiyo mimi kwa nafasi yangu nikaendelea kujisukuma na kusema kweli niliipenda shule japo umasikini ulikuwa ni sehemu ya maisha yangu.
Nakumbuka nilisoma darasa la kwanza mpaka la saba sikuwahi kuvaa viatu. Nilitembea peku, maisha yalikuwa magumu sana. Hata nilivyomaliza masomo yangu ya msingi sikubahatika kufaulu, kwa hiyo ilinilazimu nirudie darasa tena mpaka hapo nilipopata nafasi ya kufaulu ya kuendelea na kidato cha kwanza.
Lakini huko kote nilikokwenda hali ilikuwa ngumu, ada nilikosa ilinilazimu nifanye vibarua vya kulima kwa walimu wangu wa sekondari ili niweze kujikimu kimaisha, lakini maisha yaliendelea mpaka leo.
Lakini kipindi chote cha masomo yangu hadi kidato cha tano na sita nilipambana na maisha, napikia watoto nyumbani, maana dada yangu aliolewa na mama yangu aliugua miguu kwa miaka minne.
Kwa hiyo kipindi chote cha kusoma kwangu nililima ili niweze kujilipia ada huku nikijua kwamba siku moja nitafaulu, sikuwahi kukata tamaa. Pamoja na kufaulu kuingia kidato cha tano, nako hali ilikuwa ngumu kuweza kulipa ada.
Nikachukuliwa na binamu yangu akaanza kunifundisha shughuli ndogondogo za biashara ambazo zilinisaidia kupata fedha na kuendelea na elimu yangu ya kidato cha tano. Baada ya kumaliza elimu yangu ya kidato cha sita nilibahatika kuendelea na elimu ya Chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini nikichukua fani ya uchumi.
Baada ya kumaliza elimu yangu pale chuoni, nilibahatika kuisaidia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa utaratibu wa kujitolea kama mchumi, na mwisho nikaamua kufanya shughuli zangu binafsi huku nikijishughulisha na siasa.
Hayo maisha yalinipelekea mimi kuchukia kabisa mfumo wa kiserikali, nikajikuta napenda upinzani kwa sababu nikaona upinzani ndiyo tunaofanana.
Niliona jirani zangu watoto wao wakisoma shule binafsi, maisha yao mazuri, wanakula vizuri wakati wengine nikiwamo mimi, tukiwa na maisha magumu. Hali hiyo ilinifanya nikachukia sana mfumo wa maisha wa namna hiyo.
RAIA MWEMA: Uamuzi wa kuwania nafasi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam ulikuwa ni wako binafsi au chama chako cha Chadema kilikutaka ufanye hivyo?
ISAYA: Ulikuwa ni uamuzi wangu mwenyewe. Nilitaka kuwania udiwani ili nije kugombea nafasi ya umeya, kabla hata sijawa meya baadhi ya wanachama wetu walishaanza kuniita Meya.
Hata mratibu wangu wa chama alikuwa akiniita Meya hata kabla sijatangaza kuwania nafasi hiyo. Nakumbuka hata wakati wa kampeni mwaka 2015, aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji, alikuja Kigamboni kufanya kampeni na sikutambulishwa kama mwenyekiti wa Chadema Kigamboni bali nilitambulishwa kama Meya mtarajiwa kama vile watu walikuwa wakiotea maisha yangu ya baadaye.
RAIA MWEMA: Kabla hujawa Meya, ni mambo gani ulikuwa ukitamani yabadilike hapa Dar es Salaam?
ISAYA: Kama nilivyotangulia kusimulia juu ya maisha yangu, siridhishwi na huduma zilizokuwa zikitolewa na serikali, hasa huduma za jamii. Suala la shule, hususani kipindi ambacho kwa Dar es Salaam watoto wengi shuleni kote wanakaa chini. Unaenda shuleni, kwa bahati mbaya shule nzima ina watoto 400, darasa moja lina watoto 250. Nilikuwa nikifika pale nilirejea maisha niliyopitia, ilikuwa inaniuma sana, nikawa natamani wananchi wanisaidie mimi kuwa diwani ili niwasaidie.
Niwasaidie si kwa kutafuta fedha ya serikali bali ningechangisha Watanzania wenzangu kuwahamasisha ili angalau tuweze kununua madawati. Naomba nikwambie jambo moja ambalo wengi hawalifahamu kwamba baada tu ya kuchaguliwa nilijenga madarasa saba kwa mwezi mmoja huko katika kata yangu ya Vijibweni, Kigamboni.
Nilifanya hivi baada ya kuwahamasisha wananchi kuchangia kwa kushirikiana na kampuni mbalimbali. Maadam nimekuwa Meya, sitaki kusikia vilio vya madarasa na madawati katika jiji hili.
RAIA MWEMA: Kwa nafasi yako ya Umeya, unadhani ni changamoto gani kubwa inayokabili jiji na namna unavyofikiria kupata utatuzi wake?
ISAYA: Changamoto ambayo naiona ni huduma za jamii ambazo nimetangulia kuzisema kwa upande wa elimu na afya. Kwa mfano, unaweza kwenda hospitalini unakuta mama amelala chini baada ya kujifungua.
Jambo hili linashindwa kabisa kuniingia akilini kwa sababu jiji hili lina vyanzo vingi vya mapato. Naomba kutumia nafasi hii kuwaomba wahisani wa ndani na benki zetu kujitolea kutusaidia.
Dar es Salaam ni mji maarufu na muhimu hapa nchini. Tunazo benki, hawa wanaosimamia benki hizi wengi wao wamesoma maisha ya shida kweli lakini wamefika sehemu wamejisahau. Yaani nchi hii imefika mahali ambapo hakuna mtu anayejali mtoto wako kukaa chini. Hakuna mwenye kutaka kujua kwa sababu watoto wao wote wamewapeleka katika shule za kimataifa.
RAIA MWEMA: Najua una mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu. Katika mwaka huu wa 2016, ni mambo yapi unadhani utakuwa umeyatekeleza kufikia mwisho wa mwaka?
ISAYA: Kwanza ninapata wakati mgumu sana kuahidi kwa sababu sijaitisha bado kikao cha Baraza la Madiwani. Unajua unaahidi kile ambacho kimeshapitishwa na baraza hilo. Sasa hivi naweza kuahidi kitu na baadaye baraza likaja kunigomea kwa sababu ule ni mjadala unaendeshwa.
Nadhani tutakuwa na mjadala mzuri ndani ya Baraza la Madiwani na pale tutakubaliana kuhusu kipaumbele. Kipi kitaanza na yapi yatafuata.
Kwa hiyo tutakapokutana tutakubaliana utekelezaji wa vipaumbele vyetu. Nadhani siku zijazo, pengine baada ya Aprili 18 wakati madiwani wote watakapokutana, tutakuwa tumeshapata kitu cha kuwaambia na namna ya utekelezaji wake.
RAIA MWEMA: Una maoni gani kuhusu mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (DART) na namna gani utasaidia kuhakikisha huduma hii inanza haraka iwezekanavyo?
ISAYA: Kama unavyofahamu nina siku ya tatu tangu niingie ofisini (Aprili 1, 2016), hivyo sijapata ripoti yoyote, tutakapokaa pamoja na menejimeti watanipa taarifa.
RAIA MWEMA: Dar es Salaam inakabiliwa na kero ya maji kwa upande wa baadhi ya maeneo, ikiwemo Ubungo, Kimara, Mbagala na maeneo mengine pembezoni mwa jiji. Ni namna namna gani umejipanga kumaliza changamoto kwa wananchi wa Dar es Salaam?
ISAYA: Kwanza lazima tukubali kwamba kuna miradi ambayo inaendelea. Nimepata taarifa kwamba mradi wa Ruvu Juu sasa hivi uko vizuri, mradi wa Kwembe pia unakwenda vizuri.
Inawezekana mwaka huu kwa mujibu wa maelezo ya mainjinia, maji yanaweza kupatikana kwa Jimbo la Kibamba, Ubungo, Kawe na Segerea.
Lakini kuna watu ambao huu mradi unawaacha kwa mfano watu wa Mbagala na Kigamboni lakini nafahamu kwamba kuna mradi wa maji wa Kimbiji ambao maeneo haya ndiyo yanauhusu. Lakini kwa kuwa wamenichagua mimi Isaya Mwita kuwa meya wao, basi mradi wa Kimbiji utatekelezeka.
RAIA MWEMA: Kulikuwa na figisufigisu nyingi wakati wa mchakato wa kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Utafanya nini kuhakikisha kunakuwa na mshikamano katika baraza litakalokuwa likikutana?
ISAYA: Nimeshasema na ninarudia kusema kwamba mimi au sisi tumekwishafika hapa, tunataka tufanye kazi. Watanzania wanataka maendeleo, nasi Ukawa tumepewa miaka mitano na baada ya miaka mitano hii na CCM hao unaowaona watasimama na kusema kwamba, tuliwaambia kwamba hawa watu hawafai, tungewapa nchi ingekuwaje?
Tumewapa Dar es Salaam, wamefanya nini? Kwa hiyo ninapaswa kutoa matokeo chanya, nataka nifanye kazi naomba mlipe kodi.
Nawaambia wana Dar es Salaam, kwa yule anayepaswa kulipa kodi ya majengo, na kodi nyingine mbalimbali lazima walipe.
Tumesema tutakuwa tunawatangazia kila makusanyo na namna yalivyotumika. Na baraza langu naomba niwaambie waandishi wa habari litakuwa linatangazwa. Hata tunaloliandaa litatangazwa kwenye vyombo vya habari. Mje mshuhudie, ni utaratibu mpya, na ndivyo kanuni inavyotaka. Ningekuwa na uwezo ningerusha moja kwa moja kupitia televisheni na redio nchini.
RAIA MWEMA: Kipindi mnajiandaa kuchagua Meya kulikuwa na tetesi kwamba sakata la UDA ilikuwa ni kikwazo kwa Ukawa kupewa jiji. Kwamba chama tawala hakikuwa kinataka mpate fursa ya kuibua yale yasiyopaswa kujulikana. Je, ni namna gani mmepanga kushughulikia suala la UDA?
ISAYA: Faili la UDA nimeletewa na tayari liko hapa mezani kwangu, naanza kulisoma leo. Sasa niseme nini tena hapo? Nimepanga kwamba nitasoma kila ukurasa kwa umakini wa hali ya juu. Tutasaidiana na wanasheria wa ndani na wa nje kama kutakuwa kuna lazima ya kufanya hivyo ili Watanzania wajue shirika lao likoje. Lakini pia naamini haki itatendeka.
RAIA MWEMA: Nje ya siasa unapenda mambo gani?
ISAYA: Nje ya siasa, kwanza nampenda Mungu sana. Lakini mbali na hapo pia napenda mpira unaochezwa nje ya nchi na ndani pia. Mimi ikifungwa timu ya Simba huwa napata machungu sana lakini sina namna ya kufanya.
RAIA MWEMA: Dar es Salaam ni moja ya maeneo ya hapa nchini yaliyokithiri kwa uingiaji wa dawa za kulevya pamoja na matumizi yake. Umejipanga vipi angalau kupunguza kasi ya uingiaji kama si kumaliza kabisa?
ISAYA: Hili suala naamini vyombo vya usalama vinashughulikia. Tuna idara ya usalama wa taifa, wao hawa wana wajibu kwa sababu kimsingi wanawajibika kwa Rais wa chi, nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria.
RAIA MWEMA: Unawaambia nini wananchi wa Dar es Salaam ambao wamewekeza matumaini kwako ili kuhakikisha jiji hili linakuwa mahala salama pa kuishi?
ISAYA: Wana Dar es Salaam naomba niwaombe sana, wanisaidie kulipa kodi. Tunaandaa utaratibu ambao utawezesha wao kulipa kodi, wasijisikie wanyonge, walipe, fedha zao tutazitumia vizuri.
Tukiweza kukusanya fedha vizuri tutaweza kufanya mambo yatakawapa usalama wa kiafya, kiuchumi, kijamii na kimiundombinu.
Ili wawe salama barabarani, ni lazima barabara ziwe nzuri. Hilo linahitaji fedha. Ili wawe salama kiafya, inabidi wakae sehemu zilizo salama na huduma za hospitalini na kwenye vituo vya afya ziboreshwe. Hilo linahitaji fedha.
Fedha hiyo itapatikana kutoka kwa wananchi wenyewe kupitia kodi zao.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/meya-wa-dar-nilitembea-peku-kwenda-shule-miaka-saba-1#sthash.B8M0qjFA.dpuf
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment