Mzozo wa kidiplomasia unatokota
baada ya Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kunaswa kwenye Kamera
akimwambia Malkia Elizabeth wa Pili kuwa viongozi wa mataifa mawili
yenye ufisadi mkubwa kote duniani Nigeria na Afghanistan watakuwa
miongoni mwa wageni waalikwa katika kongamano la kupambana dhidi ya
zimwi la ufisadi litakalofunguliwa siku ya Alhamisi mjini London.
Matamshi
hayo ya Cameron yalitolewa katika kasri la Buckingham bw Cameron
alipokuwa amekwenda kumtembelea malkia Elizabeth katika sherehe ya
kuadhimisha miaka 90 ya kuzaliwa kwake.Aidha Cameron alieelezea malkia Elizabeth jinsi mataifa hayo yalivyosakamwa na viongozi mafisadi.
Kiongozi wa kanisa la kianglikana Askofu mkuu wa Canterbury Justin Welby aliyekuwa na viongozi hao wawili anasikika akimkumbusha Waziri mkuu bw Cameron kuwa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari si mfisadi.
Afghanistan iliorodheshwa katika nafasi ya 167, nafasi moja pekee mbele ya Somalia na North Korea, katika orodha ya 2015 ya shirika la kupambana na ufisadi duniani Transparency International .
Nigeria iliorodheshwa katika nafasi ya 136.BBC
0 comments:
Post a Comment