Bunge limempitisha Mhe Azzan Mussa Zungu (MB)-Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, kuwa Mwenyekiti Wabunge kuziba nafasi
iliyoachwa wazi baada ya Mhe Spika kufanya Mabadiliko ya Wajumbe wa Kamati za
Kudumu za Bunge.
Awali kabla ya Jina la Mhe Zungu kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya
kuthibitishwa, Kamati ya Uongozi chini ya Uongozi wa Spika wa Bunge Mhe Job(MB)
Ndugai ilikutana na Wajumbe wote kwa kauli moja walimteua Mhe Zungu kuziba
nafasi hiyo.
Akizungumza wakati wa kikao cha Bunge cha Jioni Katibu wa Bunge Dkt
Thomas Kashililah alisema kuwa baada ya
Kamati ya Uongozi kumteua Mhe Zungu kuziba nafasi hiyo kinachofuata ni
Uchaguzi.
Hata hivyo Dkt Kashililah kwa kuwa Mhe Zungu ndiye mgombea pekee
wa nafasi hiyo ni dhahiri kuwa anapita bila kupigwa na hivyo akamuomba Naibu
Spika Dkt Tulia Ackson (MB) ambaye ndiye
aliyekuwa anaongoza kikao hicho amtangaze Mhe Zungu kuwa Mweyekiti Wabunge.
Mara baada ya Naibu Spika kumtangaza Mhe Zungu kuwa Mweyekiti
Wabunge alimkaribisha ili aweze kuwashukuru Wabunge huku akimuambia kuwa makofi
ambayo Wabunge wote na wa pande zote walikuwa wanapiga ni ishara kuwa wana
imani kubwa na yeye.
Akitoa shukrani kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe Zungu
alisema kuwa anafahamu kuwa kazi iliyopo mbele yake ya kumsaidia Spika Wabunge
ni kubwa na nzito lakini akaahidi kuwa ataaifanya kwa ufanisi na bila
upendeleo.
Mhe Zungu anaungana na Wenyeviti wengine ambao ni Mhe. Andrew Chenge (MB) – Mwenyekiti, Kamati ya Sheria na Mhe.Najma Giga (MB)-Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba ambapo wote watatu na pamoja na Naibu Spika watamsaidia Spika kuongoza mhimili wa Bunge. Wenyeviti wote watatu watahudumu katika kuliongoza Bunge la Kumi na Moja katika kipindi cha Nusu ya Uhai wake kabla ya uchaguzi mwingine kufanyika.
0 comments:
Post a Comment