mwanazuoni

TED CRUZ KUMZUA TRUMP LEO ?



Ted  Cruz kumzua  Trump  leo? 
Leo ni siku ambayo  huenda tukaanza kumjua  mgombea atakayepeperusha bendera nyekundu ya chama cha Republican dhidi ya bluu ya Democratic   hapo mwezi  Novemba katika uchaguzi mkuu wa Marekani. Leo  wanachama wa Republic  katika jimbo la Indiana wanatarajia kupiga kula kuchagua  wawakilishi  57 wanao waniwa na wagombea watatu  yaani Donald Trump seneta wa New York, Ted Cruz seneta wa Texas na John Kasch gavana wa Ohio. Ili kujihakikishia tiketi  ya kugombea kupitia chama cha Republican  mgombea anatakiwa  kupata wajumbe 1237 mpaka sasa Donald Trump anaongoza kwakupata wajumbe wengi  996 akifuatia  Ted Cruz  565 huku  John Kasch akishika mkia  157. Ifahamike kuwa  Indiana ndio jimbo  lenye  wajumbe wengi mbali na Calfonia lenye wajumbe 172. Hivi karibuni Cruz na Kasch walikubaliana kuunganisha nguvu  kwenye jimbo hilo la Indiana  ili kumzuia Trump asipate  wajumbe 1237 wanaohitajika kupata tiketi ya kugombea. Wawili hao hawana nafasi yakupata wajumbe 1237  hata wakishinda  kwenye majimbo yalio salia badala yake wanamatumaini ya kupata tiketi ikiwa mshindi wa mojakwamoja kupitia wapiga kura atakosekana. Hivyo kurefusha mchakato mpaka kwenye  kongamano la Cleveland   linalofayika hapo mwezi  Julai. kongamano hililo humchagua mtu atakaeonekana anafaa kwenye chama cha Republican.  Hata hivyo huenda  jina la Trump lika katwa kama mchakato wa kumpata mgombea utaamuliwa na kongamano la Cleveland kwani Trump haungwi mkono sana na wajumbe wengi wa Grand Old Party  (GOP ). Hivyo kuufanya  uchaguzi  katika jimbo la Indiana kuwa muhimu sana kwa  Donald Trump kukwepa ko ngamano la Cleveland  na pia kwa  Ted Cruz na John Kasch wanaotegemea  Kongamano la Cleveland  ili kupata tiketi ya kupeperusha bendera  nyekundu ya wahafidhina wa chama cha Republican.
Mwandishi Morgan

Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment