BAVICHA WAPUUZA KAULI ZA MAKONDA,WASISITIZA UKUTA UPO PALE PALE
Ikiwa ni siku moja tu kupita Tangu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda Kuwaagiza askari wa FFU na viongozi wa ulinzi ndani ya Dar es salaam kuhakikisha wanazima haraka mipango yote inayofanywa na chama cha CHADEMA ya kutaka kufanya mikutano katika operationi yao waliyoipa jina la UKUTA,hatimaye Uongozi wa baraza la vijana Chadema BAVICHA wameibuka na kupuuza agizo hilo huku wakisisitiza kuwa maandalizi ya kuelekea September moja yamekamilika na watanzania wajiandae kudai haki yao.
Akizngumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Bavicha Taifa PATROBAS KATAMBI amesema kuwa kauli ya mkuu wa mkoa ni ya kupuuzwa kwani hana mamlaka kisheria sio tu kuzuia mikutano bali hata kuruhusu bali mwenye mamlaka hiyo kisheria ni OCD hivyo watanzania wasitishwe na wajitikeza kwa wingi.
Amesema kuwa wao kama Vijana wa chadema walipokea agizo la viongozi wao wakuu wa chama la kufanya maadalizi ya kufanya mikutano nchi nzima ifikapo September moja na wao wakaanza maandalizi mara moja na tayari maandalizi hayo yamekamilika na wanajiandaa kufanya mikutano hiyo.
Chama cha CHADEMA kimepanga kufanya mikutano yake nchi nzima ifikapo September Moja kwa lengo la kupinga mfumo unaotumika na Serikali ya awamu ya Tano wanaodai kuwa ni mfumo wa Kidikteta na operation hiyo imepewa jina la UKUTA.Mpaka sasa mikutano hiyo imeanza kupigwa marufuku na viongozi wa serikali akiwemo Rais magufuli na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam lakini CHADEMA wanasisitiza kuwa watafanya mikitano hiyo
0 comments:
Post a Comment