Watu wenye ushawishi pamwe na wanasiasa maarufu nchini Marekani kutoka katika bunge la Congress na chama cha Republican wametoa matamko yao kuwa hawatampa kura zao mgombea wa nafasi ya urais Donald Trump, wakisema kwamba mgombea huyo hatoshi kwa nafasi hiyo nyeti ulimwenguni.
Mapema wiki hii, Richard Hanna kutoka mjini New York amekuwa mwanachama wa kwanza kutoka chama cha Republican kutamka hadharani kuwa atampa kura yake mgombea wa kiti cha urais kutoka chama cha Democrat Hillary Clinton.
Hanna amemwita Donald Trump aibu ya taifa, wanachama wengine kutoka chama cha Republican wamejitenga kutomshabikia Trump ama hata kutomuunga mkono.
Kauli za Donald Trump,sera zake dhidi ya wanawake,masuala ya wahamiaji wasiokuwa na nyaraka zinazotakiwa na Waislamu hayawaingii kichwani viongozi walio wengi kutoka upande wa chama cha Republican.
Katika hatua nyingine rais Barack Obama amemshambulia mgombea huyo wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwa madai ya kutokuwa na sifa stahiki kuwa rais wa Marekani.
Obama hakuishia hapo bali amewashangaa wafuasi wa chama cha Republican kwanini wanendelea kumuunga mkono mgombea huyo, amesema kwamba Trump amekuwa ni tofauti na wagombea waliopita wa chama cha Republican kama alivyo Mr Trump namna anavyotoa hukumu ama tabia zake za kuajabisha ambazo haziendani na mtu anayetarajiwa kuchukua madaraka makuwa na yenye nguvu kubwa zaidi katika dunia.
Naye Donald Trump hakuacha maneno hayo yapite bure bali alijibu mashambulizi kwa kumshutumu raisi Barack Obama kama kiongozi aliyeshindwa na kwamba mgombea anayetaka kurithi nafasi yake Hillary Clinton, naye hafai kuwania nafasi hiyo ama hata katika ofisi yoyote ile ya serikali.
WAKATI HUO HUO
Wakati vita vya maneno katika kampeni hizo vikipamba moto, mkuu wa kamati kuu ya chama cha Democratic nchini Marekani amejiuzulu nafasi hiyo. Uamuzi huo wa Amy Dacey kujiuzulu unafutia kuvuja kwa maelfu ya barua pepe zenye kuonesha mapendekezo ya chama cha Democratic dhidhi ya njama za makusudi za kudhoofisha kampeni ya Hillary Clinton dhidi ya mpinzani wake wa zamani Bernie Sanders aliyekuwa mgombea urais.
Dacey kuachia ngazi kwake anakuwa mtu wa pili kujiuzulu baada ya mwenyekiti wa wanawake wa chama hicho , Debbie Wasserman Schultz,kabla ya mkutano mkuu wa taifa wa chama cha Demokratic mjini Philadelphia wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment