mwanazuoni

MO AIPA SIMBA SC 100 MILLION KWA AJILI YA USAJILI

Mkurugenzi Mtendaji na rais wa makapumni ya Mohammed Enterprises Ltd (MeTL Group) Mohammed Dewji ‘MO’ ametoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa klabu ya Simba kwa ajili ya kusaidia zoezi la usajili kama alivyoahidi siku chache zilizopita.
Bilionea huyo ambaye anania ya kuwekeza bilioni 20 alisema, yuko tayari kusaidia zoezi la usajili endepo klabu hiyo ingeridhia kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wanachama wa kadi hadi kuwa kampuni ambayo itaendesha kwa mfumo wa kibiashara.
Julai 31 klabu ya Simba iliridhia kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji japo haikujulikana mara moja kwamba wameamua kuingia katika mfumo upi.
MO amesema ametimiza ahadi aliyoitoa baada ya wanachama wa klabu ya Simba kukubali kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji: “Niliahidi kusaidia kwenye zoezi la usajili kwa ajili ya klabu yetu ya Simba SC, ninafuraka kubwa sana kumkaribisha rais wa klabu (Simba). Mimi kama mwanachama ningependa kuchangia kwenye hilo zoezi.”
Rais wa Simba Evans Aveva ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Patrick Kahemle, amemshukuru MO kwa kuamua kusaidia zoezi la usajili ambalo bado klabu hiyo inakabiliwa na upungufu wa mkwanja kwa ajili ya usajili licha ya Mbunge huyo wa zamani wa Singida kutoa shilingi milioni 100 kupiga tafu usajili.
“Kama alivyoahidi kwenye mkutano na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya mkutano wetu mkuu, aliwaambia wana Simba kupitia waandishi wa habari kwamba endapo mkutano wa August 31 utaridhia mabadiliko ya uendeshaji wa klabu yetu, basi yeye kama mwanachama wa Simba atachangia zoezi la usajili.”
“Usajili wetu wa Simba unaendelea haujafika mwisho tumebakiza takribani siku tano ili kufunga zoezi hilo, ni zoezi ambalo lina gharama kubwa. Tuliwasiliana na mwanachama wetu tukamwambia kiasi kilichobaki ambacho ni shilingi milioni 420 ili kumalizia zoezi hili la usajili. Kwahiyo alichotoa mwanachama wetu kitatusaidia kwa kiasi kibwa kutoka hapa tulipo.”
“Kuna mchezaji mmoja kutoka Ivory Coasta ambaye dau lake la usajili ni zaidi ya milioni 100, kwahiyo kwa kupata pesa hizi naamini tutaweza kumsajili mchezji huyo.”
“Wanachama wengine waige mfano wa Mohammed Dewji na kuchangia katika zoezi hili wasijewakasema MO ametoa kiasi cha pesa kwahiyo ndiyo tumemaliza zoezi la usajili.”
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment