Aliyekuwa waziri mkuu nchini Portugal Antonio Guterres anatarajiwa kuwa katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa UN ,kulingana na wajumbe wa umoja huo.
Bwana Guterres mwenye umri wa miaka 66,''alipendelewa na wengi '',balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitaly Churkin alitangaza siku ya Jumatano.
Kura ilio rasmi itafanyika katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi kuthibitisha uteuzi huo.
Kiongozi huyo aliungwa mkono na mataifa yaliopo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa
Bwana Guterres ,ambaye aliongoza shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi kwa kipindi cha miaka 10 atachukua mahala pake ban Ki-moon mapema mwaka ujao.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment