Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anamuhitaji kiungo wa kati Yaya Toure lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na ajenti wa mchezaji huyo.
Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 33,amecheza mara moja msimu huu,katika kombe la vilabu bingwa .
Baadaye aliwachwa nje katika kinyang'anyiro hicho.Dimitri Seluk alidai kuwa Toure amefedheheshwa na uamuzi huo.
Alipoulizwa iwapo Toure angecheza katika kombe la ligi katika uwanja wa Old Trafford ,Guardiola alisema: Unajua hali ilivyo.
Raia huyo wa Uhaspania alisema mnamo mwezi Septemba kwamba Seluk lazima aombe msamaha,iwapo Toure anahitaji kucheza katika kikosi cha kwanza ,lakini ajenti huyo aliambia BBC Sport wakati huo kwamba: Ni nini ninachofaa kukiombea msamaha?Anafaa kuongea na Yaya anayemfamnyia kazi yake''.
Na huku kukiwa hakuna msamaha uliotolewa ,hakuna mapatano kati ya mkufunzi huyo na mchezaji wake.
0 comments:
Post a Comment