Mamia ya watu nchini Iraq wanatibiwa kutokana na athari za gesi ya sumu baada ya kinu cha kemikali aina Sulphur kuteketezwa moto katika mapigano na Islamic State.
Wanajeshi wa Marekani katika kambi ya jeshi karibu na mji uliopo kaskazini Iraq, Mosul walilazimika kujifunika nyuso zao kujikinga dhidi ya moshi huo wa sumu.
Wanasema wapiganaji wa IS waikiteketeza moto kinu hicho mapema wiki hii, walipokuwa wanatoroka kufikiwa na vikosi vinavyoiunga serikali mkono katika ngome yao Mosul.
Walichukua tahadhari hiyo baada ya upepo kuusukuma moshi kutoka kwenye moto kuelekea kwenye kambi ya jeshi la anga ya Qayyarah.
Mjini Baghdad, jitihada za Uturuki kujiunga na mashambulio dhidi ya Islamic State hazikufua dafu.
Wakati huo huo, vikosi vinavyosogea vya Iraq vimeingia mji wa Qaraqosh, kilomita 32 kusini mwa Mosul, mji mkuu unaodhibitiwa na IS.
Qaraqosh, ambao ndio mji wa Iraq ulio na idadi kubwa ya waumini wa kikristo kabla ya vita unaarifiwa kuwa mtupu, hauna watu lakini wapiganaji wa IS wametega mabomu ya ardhini katika njia za kuelekea mji wa Mosul.
Wanamgambo hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio ya kujitoa muhanga katika maeneo mengine, wakiendesha magari kwa kasi kubwa yaliohamiwa kwa milipuko yakivurumizwa katika maene yanayodhibitiwa na vikosi vya serikali.bbc
0 comments:
Post a Comment