Rais wa Rwanda ,Paul Kagame ameonya kuhusu makabiliano na Ufaransa kufuatia tangazo la wachunguzi wa Ufaransa kwamba watafungua upya uchunguzi kuhusu mauaji ya aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana.
Kutunguliwa kwa ndege yake iliokuwa na wafanyikazi wa Ufaransa mwaka 1994 ilizua mauaji ya kimbari ambapo mamia ya maelfu waliuawa ,hususan watu wa kabila la Tutsi .
Uchunguzi huo umeanzishwa upya ili kupata ushahidi kutoka kwa jenerali aliyetoroka Rwanda Faustin Kayumba Nyamwasa ambaye anasema kuwa rais Kagame alihusika .
Mwaka 2006,Rwanda ilikata uhusiano wake na Ufaransa kwa miaka mitatu baada ya jaji kumtaka rais Kagame kujibu mashtaka.#BBC
0 comments:
Post a Comment