mwanazuoni

Rooney: ni wakati mgumu kuwekwa benchi England

Nahodha wa timu ya taifa ya England Wayne Rooney, amesema huu ni wakati mgumu kwake baada ya kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza kitachocheza mchezo kuwania kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Slovenia leo hii jumanne.
Kocha wa muda wa kikosi hicho Gareth Southgate, amesema uamuzi wa kumuweka benchi mchezaji huyu ni wa kiufundi na sio suala la ubora wa kiwango cha Rooney.
Nyota huyu mwenye umri wa miaka 30, anaendelea kuwa nahodha wa timu ya taifa lakini katika mchezo wa dhidi ya Slovenia, Jordan Henderson, ndie atavaa kitamba cha unahodha.
Rooney, ndie mfungaji bora wa kihistoria wa England, akiwa na bao 53 akifuatiwa na sir Bobby Charlton, aliefunga bao 49.
Pia ndie mchezaji wa pili kuichezea mechi nyingi nchi yake akiwa amecheza mechi 117 nyuma ya kipa peter shilton aliyecheza mechi 125.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment