mwanazuoni

Merkel azindua jumba la Nyerere Addis Ababa

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jumba jipya makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la rais mwanzilishi wa taifa la Tanzania, Julius Nyerere.
Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.
Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.
Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.
Jumba hilo afisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.
Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.
Mwalimu Nyerere alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).BBC 
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment