Shambulio limetokea eneo maalumu la ibada la waumini wa dhehebu la shia katika mji wa Kabul huko Afghan.
Watu 14 wamekufa na wengine 26 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Shambulio hilo lilitokea katika mkusanyiko wa washia waliokua wakiadhimisha siku muhimu ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein katika kalenda ya Shia, inayojulika kama Ashura.
Mashuhuda wanasema kuwa mlipuko ulisikika kabla ya mshambuliaji kumimina risasi. Wasuni wenye msimamo mkali kama Taliban wanaamini kuwa washia ni waasi na wanalenga misikiti na mikusanyiko ya Umma.
Mpaka hivi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lilitangaza kuhusika na shambulio hilo,
0 comments:
Post a Comment