Mgombea urais wa chama cha Republican Marekani Donald Trump amewaambia wafuasi wake kuwa shutuma za kukashifu wanawake ni njama ya kumfanya ashindwe uchaguzi wa Marekani.
Katika mkusanyiko na wafuasi wake huko Florida Trump amekanusha kuwa tuhuma hizo ni uongo.
Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo Trump anaonekana kushindwa dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton.
Mapema mke wa Rais bi Michelle Obama amemshambulia Trump na kusema kuwa kitendo cha Trump cha Udhalilishaji wa wanawake ni cha Kushangaza na kutisha
0 comments:
Post a Comment