mwanazuoni

MADARAKA YA KIFALME YA WAZIRI WA HABARI KWENYE MUSWADA WA HUDUMA ZA HABARI


“…Unapoandika sheria mpya maana yake ni kwamba sheria ambayo ipo wakati huo au mazingira ya wakati huo hayatoshelezi hali ambayo ilitakiwa kuwapo. Sheria hii ambayo tunaijadili leo lengo lake ni kujibu malalamiko ya muda mrefu kuhusiana na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976. Lakini, katika mambo yote ya Sheria ya Magazeti jambo ambalo lilikuwa linalalamikiwa sana ni suala la mamlaka ya Waziri kufungia gazeti lolote au chombo chochote cha habari muda wowote ambao yeye anataka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 kifungu cha 25 kinasema ‘Minister may prohibit publication of the Newspaper’. Tulitarajia kwamba Sheria hii mpya ingekuja na provision bora zaidi miaka 40 baada ya Sheria ya 1976 kutungwa. Lakini Mh. Mwenyekiti, kifungu cha 55 cha Sheria Mpya ambayo tumeletewa hapa ambacho kinasema ‘powers of the Minister; The Minister shall have power to prohibit or otherwise sanction the publication of any content…not any newpaper!..any content that jeopardizes national security or public safety’. National security au public safety haijawa-defined pahala popote.
Sheria ya mwaka 1976, kifungu ambacho kinamwezesha Waziri kufungia gazeti kimeweka hata masharti ya namna ya kufungia. Sheria ya Mwaka 2016 kifungu hicho kimetoa tu powers na Waziri anaweza kuamua  tu kufanya anavyotaka. Kwa hiyo, hakuna ubora wowote kati ya Sheria hii (Ya Mwaka 1976) na Sheria Mpya ambayo tunataka tuitunge hivi sasa. Ndiyo maana tunasema na tunatoa wito kwa serikali kwamba kuna haja ya kufanyia kazi zaidi Mswada huu kwa sababu hatuoni tofauti kubwa..”
Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo,
Sehemu ya Mchango wake Bungeni kwenye mjadala kuhusu “Muswada wa Huduma za Habari”
Tarehe 04 Novemba 2016.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment