mwanazuoni

UONGOZI BORA KATIKA MFUMO WA VYAMA VINGI

UONGOZI BORA KATIKA MFUMO WA VYAMA VINGI
Wakati watu wanatumia muda mwingi kujadili sakata la Ubadhilifu wa fedha za Umma(TEGETA ESCROW) Mimi natumia muda mwingi kukamilisha kitabu nilichokipa jina la UONGOZI BORA KATIKA MFUMO WA VYAMA VINGI. Lengo kuu ni kuwawezesha viongozi wa sasa na vijana wenye ndoto za kuwa viongozi kwa siku za usoni kufahamu mambo ya msingi katika uongozi.
1. kiongozi ni nani,mtu wa namna gani,
2. Nini maana ya uongozi,
3. Kwa nini watu wanataka kuwa viongozi? Nini kipaumbele chao?
4. Uzalendo na uongozi bora
5. Mtiririko wa kiuongozi/madaraka, ngazi za uongozi(Chain of Command), 6. Miiko ya uongozi(Leadership ethics),
7. Uongozi na rushwa
o Nini maana ya rushwa
o Nini chanzo cha rushwa
o Nini matokeo/hasara za rushwa katika jamii na Taifa kwa ujumla
o Ni namna gani unaweza kujiepusha na rushwa
8. Uongozi bora na upana wa demokrasia,
9. Changamoto unazoweza kukabiliana nazo kwa kuwa kiongozi wa Umma,
10. Mawasiliano ya Umma na Uongozi,
11.Mbinu bora za kuendesha mikutano ya hadhara,
12. Majukumu makuu ya Viongozi wa kuchaguliwa kama Vile Diwani,Mbunge,Raisi....kwa upana wake ili kuwawezesha wagombea kufahamu majukumu yao mapema na sio kuahidi pasipo kujua anachokiahidi kipo nje ya majukumu yake
Namuomba Mungu anisaidie kufanikiwa kimaisha kwa jitihada zangu pasipo kuhujumu mali ya Umma! Viongozi wenzetu wa nchi za magharibi hufanikiwa kwa kutumia taaluma zao kwa kuandika Vitabu, uvumbuzi wa Technolojia, kufanya biashara.....lakini viongozi wa Afrika wanaona njia nyepesi ni kuchota pesa za Umma........!Ukifika wakati mwafaka ni vema vijana wenzangu mniunge mkono kwa kununua kopi za vitabu kwa wingi. Mungu ibaliki Afrika, Mungu ibaliki Tanzania.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment