Mbunge wa Jimbo la Masasi ndugu DR Rashid Chuachua ameendelea na ziara yake ya kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Jimbo lake. Siku ya jana alikuwa kata ya Sululu na amefanya mikutano miwili ya hadhara. Mkutano wa kwanza alifanya kijiji cha Magomeni na wa Pili alifanya Makurani. Wananchi walikuwa na kero nyingi zilizogusa nyanja mbalimbali lakini Kero kubwa ilijiegemeza kwenye Kilimo cha Korosho.
KUHUSU KUBADILIKA BADILIKA KWA BEI YA KOROSHO
Majibu ya mbunge yalikuwa kama ifuatavyo
kuhusu korosho bei aiwezi kuwa sawa katika minada yote kwani Korosho zinashindanishwa katika minada itategemea unalipwa shilingi gani kulingana na bei katika mnada. pia bei ya Korosho inaweza kushuka kutokana na ushindani. nitumie nafasi hii kuwaomba wale wenye korosho waende kuuza korosho kabla ya bei ya korosho kushuka zaidi. Kabla ya Christmas kutakuwa na minada miwili hivyo ni bora kupeleka mapema. wewe upo mmoja unasema unaumia nataka ni kuhakikishie kuwa mimi naumia sana kwani kwa siku napigiwa simu zaidi ya mara 1000 kuhusu kulipwa pesa za korosho. Jana tulikuwa tumefanya kikao na Mkuu wa Wilaya amesema mpaka tarehe 30.12.2016 wakulima wote wanatakiwa kulipwa pesa zao.
KUHUSU WAKULIMA KULIPWA PESA ZAO
kwanza kuna shirika linakagua hesabau za vyama vya msingi linaitwa COWASCO. Tayari lipo kwenye mpango wa kufutwa na litafutwa kwa sababu watu wa vyama vya msingi wakiiba fedha wanawahonga Cowasco na Cowasco hawatoi hesabu za kweli za wizi katika vyama vya msing.
La Pili kuhusu fedha za wananchi kwa sababu serikali imeahidi kuleta CAG Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na hatua za mwanzo zimeshachukuliwa kwa kuvunja baaadhi ya Bodi vya Vyama bado tunaendelea na utaratibu na bodi za vyama zitavunjwa na wote watakao tiwa hatiani kwa wizi watawajibika na hili tunalizungumza wazi. kwani hizi fedha azikuibwa na wanakijiji zimeibwa na mtu na huyu mtu atawajibishwa tu. katika chama cha msingi MKARAMANI kuna mengi yamefanyika na nataka niwaambie tayari kuna mgogoro wa viongozi waliopota wa vyama vya msingi walikwenda kukopa kwa bwana mmoja anaitwa James shilingi 6 million wakadanganya kuwa wanakwenda kununua Pembejeo. Kuna wengi mlikuwa mnasikia walikamatwa na polisi na kutiwa ndani. Mmesikia tayari nimeshatoa agizo kwa Polisi kuwa wafanye Uchuguzi. Wananchi wa Mkaramani walichanga kiasi cha shilingi kama 14 million kwa ajili ya kununua pembejeo. Viongozi kwa utaratibu wao na wengine wapo hapa walikwenda wakasema tunakopa shilingi 6 million kwa Bwana James za kununua pembejeo wakati wanakabidhiana madaraka baada ya kuvunja bodi. Wakachukua ile deni la shilling 6 Million wanataka bodi mpya ilipe lile deni. Bodi mpya ikasema mbona pembejeo wananchi walichangishwa inakuwaje hizi shilling 6 Million tulitewe sisi huu ni wizi mtupu.
Nimeagiza nimeagiza kwanza wale watu waachie ilo la kwanza halafu uchunguzi ufanyike wa kina kuna watu ambao wamechukua hizi pesa na kuweka mifukoni mwao halafu wanataka wakulima tena wa Mkaramani wahusike kulipa shillini 6 Million yale ya nyuma ya matreka na mambo mengine wanafikiri tumesahau na ili pia. Kwahiyo taratibu zinaendelea kuchukuliwa watakamatwa na watalipa utaratibu ndio huo.
KUHUSU MAJI
Kuhusu suala la maji ni tatizo kubwa na hata mimi binafsi linaniumiza sana. kitu pekee ambacho naomba nikiombe kwenu ni kuendelea kuwa na subiri. Ukiwa kiongozi wa kisiasa tuambiwa maneno mengi lakini mwisho wa siku watu watakuja kukupima umetekeleza au ujatekeleza. na mwisho wa siku kwetu sisi ni mwaka 2020. Hili tunalosema hapa maji yamefikia hapo ni juhudi tu za mwaka wa kwanza na kila wakati serikali inatakiwa ihakikishe inatatua tatizo la maji. Mimi nisingependa na mimi ndio nilikuwa wa kwanza kutoa ahadi na niliimba Jimbo nzima kwamba mwanamke tutamtoa ndoo kichwani ninajua ni mtu mwenye hekima zangu ninajua ulimi wangu ulitamka na nina sema nipo tayari kuadhibiwa kwa kutotimia kwa ahadi tulizoziweka kwa sababu hakuna mbunge wa milele na wala diwani wa milele. Alama tuliamua kuweka kwa mwananchi wa kata ya Sululu tutaiweka na tutafanya yale tutakayo yaweza 2020 hatuta itaji kuimba wimbo wa maji. wanasema maji yanaweza kuwepo lakini watu wakaamua kutupumzisha hivyo niseme kauli hii ni ya kawaida kwa wanasiasa.Sisi kumekulewa kaka kwani mwanasiasa ni mtu wa kuchaguliwa kwa vidole.
KUHUSU SOLAR KATIKA ZAHANATI YA MAKURANI
Niseme tu nilitegemea hata leo fundi awe amefika hii ni ahadi ninayotoa hapa sasa. na ninasema mwezi huu wa 12 ninatenga fedha itakayokuja kwa ajili ya kuweka solar. hii ni serikali ya hapa kazi tu atufanyi vitu kwa kubahatisha bahatisha nimeshazungumza na mheshimiwa diwani aje fundi aangalie lakini tathmini ndogo si chini ya Million Moja ambayo tutaitenga kwa ajili ya kuweka solar pale na tutaweka naomba tuwe na subiri kwa kuwa tumesema tutaweka na mwezi huu wa 12 tutakuja kukabidhi fedha kwa ajili ya kuweka solar sio kwa sababu ya kumpendezesha mtu lakini kwa sababu ni jukumu letu na watu wapate huduma nzuri za afya.
KUHUSU SOKO NA GHARA
Huu mgogoro nimeusika lakini ninavyojua mimi ardhi ni mali ya kijiji uongo kweli nimesikia mimi ili jambo ardhi ni mali ya kijiji na hata aliyeeleza na kulileta ili jambo kwangu hakiwa anamaana jambo ili lipo hapa hapa kijijini na wenyewe wapo hapa hapa. Kwa sababu wakati mwingine ukisema jambo wakati unalo hapo hapo unatakiwa ulitatue hapo hapo. Niendelee kusisitiza viongozi wa kijiji. Jambo ili limeanza muda mrefu na lina nyimbo jambo hili msidhani mimi silifahamu nataka niseme hadithi zake kidogo. Ninavyosikia kuna eneo ambalo shule aliitumii lakini wanakatazia nasikia tu hadithi na kuna hadithi nyingi katika hilo lakini kuna watu wabishi awataki eneo hilo litumike tu. Nawaomba jambo la ndani kwako jaribu kulitafutia ufumbuzi kwa kuzingatia kwamba shule ni mali ya kijiji ardhi ni mali ya kijiji na wananchi mali ya kijiji. Naombe jambo ili msituingize sisi wana siasa katika mgogoro kwa mambo yenu ambayo mnatakiwa myatatue kwa uangalifu wa hali ya juu. maana mnataka jambo ili mnataka kumbebesha Mtalika hapa mnataka Kunibebesha mimi namtafikisha kumbebesha Magufuri litatueni kwanza hapa ndani kuna nini? kwa maana hiyo mimi nadhani nitatumia fursa ya kukaa na uongozi wa hiki kijiji ili lilisikilize liniingie akilini kwanza naomba niseme tutaendelea kuliangalia na mimi nitalisikiliza vizuri kwa sababu mara ya kwanza nilisema mbona jambo la kijiji kwa nini lisitatuliwe na kijiji? kama ni soko ni maendeleo ya kijiji kama ni ghara ni maendeleo ya kijiji? kwani hilo ghara la mtu? kwani shule ya mtu? kwani soko la mtu? naomba jambo ili lisitupeleke katika kipindi cha kuonekana sisi wansiasi tunataka kulikorofisha nataka liishe na mimi nitaanza kulishughulikia
KUHUSU VIKUNDI VYA AKINA MAMA
Vikundi vya hakina mama kwenye hotuba yangu nimezungumza mwanzo na niseme tu kwamba yale niliyoyazungumza tuyazingatie. ingawaje na mimi nitapata fursa pia nikimaliza ziara yangu hakina mama ziara yangu ya jimbo. Nitaanza kushukuru kwenye Jumuhiya ya UWT haya tutayazungumza kwa kina sana tutayazungumza kwa kina sana. Lakini kama kuna jambo kama lile ulilisema mama kwamba umeambiwa utapata mkopo na kwa nini ajauingiziwa naomba mambo mengine naomba yafike ofisini tuyazungumze vizuri kwa kina ili tujue nani alikuambia atakuingizia mkopo na kwa nini aujapata mkopo. Sawa na swali la mama kuhsu wanao alipata D mbili. Njoo ofisini nina uwezo wa kumuita afisa elimu tukazungumza.
KUHUSU MAKATO YA SHILINGI 20
Nilipata taarifa ya makato ya shilingi 20 tena niliambiwa na raia wema wa kata hii. wakanipigia simu tena wakaniambia mheshimwa mbunge tena wameshabandika katika maghara yetu. Nikasimamisha zoezi ili kwa kumpigia simu Mkurungezi na Nikaongea na Mkuu wa Wilaya. suala lenyewe lilikuwa ni mfuko wa elimu suala la mfuko wa elimu hapa kwetu atujalizanzisha, nataka kuambia kwa nini nilizuia? hapa kwetu atujalianzisha lakini katika maeneo mengi yote kuna mifuko ya elimu ili kusudu kuboresha maeneo ya shule na kutowachangisha wazazi kushiriki katika kuboresha mazingira ya shule. kwahiyo wenzetu katika majimbo mengine walikuwa wanachangisha hizi pesa na mpaka sasa wanachangia hizi fedha. Ukitaka umekate mkulima mimi nimetoka kuondoa makato na nimepiga kelele na nimeumia sana. Ukitaka kumkata mkulima fedha yake kwanza lazima mwanzoni kabisa kabla msimu aujaanza mkubaliane na wananchi mpite kwenye mikutano wananchi waone uzuri wa jambo lenyewe. wengi wakikubali unaweza kulitekeleza. Lakini uwezi tu ghafla ukasema unawakata shilingi 20 ya elimu wapi? nilizuia na nikampigia simu diwani nikamwambia hakuna makato.Sasa mzee kama umekatwa narudia tena mzee kama umekatwa njoo ofisini kwangu na nyaraka zote zinazoonyesha kama umekatwa. kama zimekata njoo tuonane kwenye ofisi yangu ulirudishiwe Fedha zako.
KUHUSU SUALA LA MAJI.
Mimi sikuwahi kuahidi suala la maji 30.10.2016 kuwa maji yatatoka labda kama niliadiwa na viongozi waliopita. Lakini narudi tena mpute muda na muendelee kutuamini. Si raisi kwa jimbo lote la Masasi kwa muda wa miezi kumi kuweza kutatua changamoto zote kwa mara moja wakati tuna muda wa miaka mitano hata serikali ya Magufuri haitoweza kila mwaka ina bajeti yake na bajeti ya pili tutatatua changamoto zinazoendelea. Nina ahidi na nina sisitiza pale umeme utawaka wa solar
KUHUSU UMEME WA REA
Nimeshasema kuwa MAKURANI ipo kwa awamu ya tatu ya REA. Naendelea kusisitiza kuwa mimi ni Mbunge wa Watu wote wale walionipigia kura na wale ambao awakunipigia kura. Ambao wakunipigia kura watatumia muda huu kunitathmini huyu jamaa anaweza na wale walionipigia kura wataendelea kunilinda na kunishauri. Ninachokiomba kwa pamoja na kwa namna yoyote ile Mbunge wa Jimbo la Masasi ni Huyu anayezungumza hapa na Diwani wa kata ya Sululu ni Yule aliyekaa pale. Tukileta mpira watacheza waliokuwa Ukawa na Waliokuwa CCM na Tukileta solar watatumia waliokuwa Ukawa na Waliokuwa CCM na UKAWA IMEKUFAA
MAKURANI OYEEEEEE
ASANTENI KWA KUNISKILIZA
17. 12. 2016
MAKURANI
Mbunge akiongea kwa unyenyekevu Mkubwa Mbele ya Wananchi wa Kijiji Cha Magomeni
Mbunge akiambatana na Diwani Kukagua Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Magomeni
Mbunge akisikiliza Kero za Wananchi kwa Umakini Mkubwa
0 comments:
Post a Comment