Katibu wa tawi la Simba (Ngurumo za Simba) Felix Makau amemtuhumu
makamu mwenyekiti wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kuwa ni mamluki wa
Yanga kutokana na Kaburu kudai kutomtambua Mzee Hamisi Kilomoni kama
mmoja wa wadhamini wa Bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba.
“Mimi namjua Kaburu ni mamluki tu wala hana uchungu na Simba, yule ni
Yanga. Akome kumdharau mzee Kilomoni,” maneno ya mzee Makau baada ya
kutoka Ikilu kupeleka malalamiko ya Bodi ya wadhamini kupinga mchakato
wa mabadiliko ya undeshwaji yanayotaka kufanywa na klabu ya Simba.
“Namshangaa hata huyu Kaburu Nyange anasema eti hamtambui Mzee
Kilomomi mimi nahisi huyu kazaliwa Tandale na wale kwa wale watu
wasiokuwa na baba, kama kweli anababa hawezi kumdharau mzee Kilomoni,
kama yeye hana baba sisi tunababa zetu.”
“Mzee Kilomono kapata uongozi akiwa mchezaji wa Sunderland na ndiye
aliyeanzisha ule mfumo wa wachezaji kujinyima posho ili kujenga klabu.”
Kutokana na mkutano mkuu wa dharura uliofanyika mwishoni mwa juma
lililopita, Bodi ya wadhamini ya klabu ya Simba December 16 walipiga
hodi Ikulu wakiongozwa na Mzee Hamisi Kilomoni kupeleka malalamiko yao
ya kupinga mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo.
“Kundi la marafiki wa Simba wanataka kuipoka Simba, nimeona kwenye
vyombo vya habari wanasema MO katoa milioni 150 kuwapa wachezaji, ni
uongo na propaganda. MO anawatega hawa wenzake wahuni kwamba
anawakopesha lakini hili ni genge lao wanataka kujinufaisha wao wagawe
hisa, tunaiomba serikali kuingilia kati, ndio maana tulienda Ikulu
kwenda kumuona mheshimiwa.”
Mzee Makau anasema hawakufanikiwa kuonana na Rais badala yake
walionana na wasaidizi wake ambao waliwasaidia kuwapa miongozo na
anaimani watafanikiwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment