mwanazuoni

MBUNGE WA JIMBO LA MASASI AWAJALI HAKINA MAMA KWA KUGAWA VIFAA VYA KUJIFUNGULIA BURE KWENYE JIMBO LAKE

Leo Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Masasi Dr Rashid M. Chuachua kupitia Katibu wa Mbunge Wakishilikiana na Halmashauri ya Mji Masasi kupitia idara ya Mipango waliendesha zoezi la kugawa vifaa vya kujifungilia kwenye Zahanati  Nne. Yaani Zahanati ya Chisegu, Jida, Mbonde na Makulani na zoezi ilo litaendelea kwenye Zahanati nyingine zilizomo kwenye Jimbo lake. Mbunge ameamua kutumia nafasi ya kuwajali hakina mama kwa kuamini maendeleo yanaletwa na Hakina mama na Hakina baba. Yenye  kama mbunge anatambua Mchango na adha wanazopata hakina mama wakati wa kukalibia au wakati wa kujifungua ndio maana amekuja na Program ya ASANTE MAMA.

Vifaa vya kujifungulia vinatolewa bure kwa hakina mama wote waliopo kwenye Jimbo lake kwa Masharti ya kuwa wakazi wanaopatikana katika kata zote zinazounda jimbo la Masasi. 

Wanachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye ofisi zote za kata,  hakina mama wajawazito na kupewa kadi iliyoandikwa Asante Mama  na kufika katika Zahanati Zote zilizomo ndani ya Jimbo la Masasi na Kupatiwa Vifaa Hivyo Bure bila ya gharama Yoyote.

Katibu wa Mbunge Akikabidhi vifaa vya kujifungulia katika Zahanati ya Mbonde.

 Daktari Wa Zahanati ya JIDA akipokea Vifaa



Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment