Dar Es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki Tindu Lissu amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na Mashtaka manne ya uchochezi.
Lissu amepandishwa kizimbani saa 6:25 na kusomewa mashtaka hayo na wakili wa serikali Kishenyi Mutalewa.
Mutalemwa amesema upelelezi wa kesi hiyo bado lakini akawasilisha maombi ya kupinga dhamana ya mashtakiwa.
Katika maombi hayo amesema Mshtakiwa Lissu anakabiliwa na kesi nyingine tatu Mahakamani hapo na kwamba ingawa yuko nje kwa dhamana lakini amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.
Hata hivyo maombi hayo yalipingwa na wakili wa Lissu Peter Kibatala akisema kuwa Mashtaka yake yanadhamana.
amesema kiapo cha kupinga dhamana kilichotolewa na mkuu wa upelelezi wilaya ya Ilala, ASP Denis Mjumba kina dosari za kisheria kwani hakikidhi masharti ya viapo.
Mabishano bado yanaendelea...
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment