mwanazuoni

UMOJA WA VIJANA WA CCM WILAYA YA MASASI WAANDAMANA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI.


Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Masasi umefanya maandamano hayo siku ya alhamisi tar22 June,2017.Pamoja na maandamano hayo ambayo yalipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Ndg Selemani Mzee,Umoja wa vijana wa wilaya ya Masasi Umempongeza Rais kwa hatua za kizalendo anazozichukua katika kuhakikisha anaokoa rasilimali za Taifa ambazo zilikuwa zikiporwa kiholela hasa madini.
Umoja huo wa vijana umemtaka Rais kuwapuuza baadhi ya watu wachache waliowaita "makuwadi wa wawekezaji wezi" ambao wanafanya kila jitihada za kukwamisha juhudi hizo kwa kuzibeza na kukejeli.Watu wa aina hii ni wa kupuuzwa na kupigwa vita na kila mzalendo wa Nchi hii.
Aidha UVCCM Masasi umemuomba Rais Magufuli kuwachukulia hatua wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wanahusika katika kuiingiza Tanzania katika mikataba mibovu ambayo inaipa hasara Nchi yetu kama ambavyo wahusika kwenye sakata la escrow wanaendelea kushughulikiwa.
CCM MPYA, TANZANIA MPYA!


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment