aidi ya watu 140 wanahofiwa kufinikwa chini ya matope katika jimbo la Sichuan kusini magharibi mwa China ,kulingana na chombo cha habari cha serikali.
Takriban nyumba 40 ziliharibiwa katika kijiji cha Xinmo kaunti ya Maoxian, baada ya upande mmoja wa mlima kuporomoka .
Vikosi vya uokoaji kwa sasa vinawasaka manusura waliofinikwa na mawe pamoja na mchanga.
Picha zilizochapishwa na gazeti la Peoples Daily zinaonyesha matinga tinga yakiondoa udongo na mawe hayo huku shughuli ya uokoaji ikiendelea.
Wanandoa na mwana wao mmoja waliokolewa na kupelekwa hospitalini baada ya makundi ya waokoaji kutumia kamba kusukuma miamba mikubwa huku wengine wakitafuta katika vifusi kulingana na chombo cha habari cha AFP kutokana na duru za utawala wa eneo hilo.
Mpaoromoko hayo yalifunga barabara ya kilomita 1.2 kulingana na ripoti za Xinhua.
Maafisa wa polisi wa eneo hilo waliambia chombo cha habari cha serikali CCTV kwamba maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kubwa ya hivi karibuni katika eneo hilo na kwamba hali ilifanywa kuwa mbaya kutokana na ukosefu wa miti katika eneo hilo.
Kuna takriban tani kadhaa za mawe, afisa wapolisi Chen Tiebo aliambia chombo hicho cha habari akiongezea: ni eneo linalokumbwa na mitetemeko ya ardhi.
Barabara katika kaunti hiyo zilifungwa siku ya Jumamosi kwa magari yote isipokuwa yale ya huduma za dharura pekee.
0 comments:
Post a Comment