Kiungo mshambuliaji wa PSG Javier Pastore, amempa Neymar namba yake
ya jezi - 10- akisema "anataka ajisikie yuko nyumbani". (Tovuti ya PSG)
Meneja
wa Real Madrid anaamini kuwa klabu yake lazima imuuze Gareth Bale, 28,
ikiwa inataka kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)
Manchester
United wanafuatilia kwa makini hali ilivyo Real Madrid na huenda
wakapanda dau la pauni milioni 90 kumtaka Gareth Bale, 28. (Daily Star)
ose Mourinho anaamini anaweza kumsajili Gareth Bale kwa chini ya pauni milioni 90. (Don Balon)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, atawasilisha maombi rasmi ya kutaka kuondoka Stamfrod Bridge. (Independent)
Wakili
wa Diego Costa ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Chelsea
baada ya klabu hiyo kupinga Costa kwenda AC Milan kwa mkopo kabla ya
kwenda Atletico Madrid mwezi januari. (Mirror)
Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Edin Hazard, 26, amewasiliana na Barcelona kuhusu kwenda kuziba pengo la Neymar. (Don Balon)
Chelsea
wapo tayari kupambana na Liverpool katika kutaka kumsajili beki wa kati
wa Southampton Virjil van Dijk, 26, kwa kutoa pauni milioni 50. (The
Times)
Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, huenda akakosa
mechi za mwanzo za msimu kutokana na hatma yake kutofahamika.
(Telegraph)
Jurgen Klopp amekuwa na mawasiliano ya karibu na Kylian Mbappe, 18,
huku Liverpool wakiendelea kumfuatilia mshambuliaji huyo wa Monaco.
(L'Equipe)
Meneja wa Everton Ronald Koeman bado ana matumaini ya
kusajili mshambuliaji mwingine, huku bado wakiendelea kumtaka Olivier
Giroud, 30, wa Arsenal. (Liverpool Echo)
Mabingwa wa Ufaransa,
Monaco, wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji
wa Arsenal, Alexis Sanchez, 28. (Sun)
Jurgen Klopp amekuwa na mawasiliano ya karibu na Kylian Mbappe, 18,
huku Liverpool wakiendelea kumfuatilia mshambuliaji huyo wa Monaco.
(L'Equipe)
Meneja wa Everton Ronald Koeman bado ana matumaini ya
kusajili mshambuliaji mwingine, huku bado wakiendelea kumtaka Olivier
Giroud, 30, wa Arsenal. (Liverpool Echo)
Mabingwa wa Ufaransa,
Monaco, wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji
wa Arsenal, Alexis Sanchez, 28. (Sun)
Kiungo wa Bayern Munich Arturo Vidal anataka kurejea Italy, baada ya kufikia makubaliano na Inter Milan. (FCInterNews)
Meneja wa Crystal Palace Frank de Boer anataka kumsajili beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 19. (Sun)
Anderlecht
ya Ubelgiji wameingia katika mbio za kumsajili beki wa zamani wa
Arsenal Thomas Vermaelen, 31 ambaye pia anasakwa na West Brom.
(Birmingham Mail)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara
zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi
usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment