mwanazuoni

Yaliyomkuta Morata yamgeukia Romelu Lukaku, awaambia mashabiki wa United “tuheshimiane”

Katika wimbo mmbaya ambao huwezi hata kuuandika ni wimbo wa mashabiki wa Manchester United kuhusu mshambuliaji wao Romelu Lukaku, ni kati ya nyimbo ambazo zimekosa heshima.
Wimbo huo umekuwa maarufu sana katika siku za usoni ambapo mwanzo ulikuwa unaimbwa na kikundi kidogo tu cha mashabiki lakini baadae wimbo huo umezagaa kwa mashabiki wengi wa Manchester United.
Wimbo wa mashabiki wa Manchester United umekuwa ukiimbwa huku wakitaja maungo ya siri ya mwanasoka huyo yalivyo, jambo ambalo limetafsiriwa vibaya na watu wengi japo United wanaliimba kwa sifa.
Tayari chama cha soka nchini Uingereza FA kikeshaionya Manchester United kuhusu wimbo huu na kuitaka klabu hiyo kutafuta namna kuona ni kwa jinsi gani wanaweza wakawacontrol mashabiki zao.
Romelu Lukaku naye anaonekana kuchoka na sasa anaomba heshima itawale kati yake na mashabiki “ni faraja ninavyoungwa mkono na mashabiki wa Manchester United na nyimbo zao #Tuheshimiane” aliandika Lukaku.
Manchester United imeshawaonya mashabiki kuhusu jambo hilo. Kama unakumbuka wiki kadhaa zilizopita mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku alionekana kutofurahishwa na nyimbo za mashabiki wa Chelsea kuhusu yeye.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment