JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/B/78 30 Aprili, 2012
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu
wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria
Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na
kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika
Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kwa waajiri mbalimbali katika
Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:
NB: Aidha, matangazo haya yanapatikana kwenye tovoti zifuatazo: www.ajira.go.tz,
www.utumishi.go.tz na www.pmoralg.go.tz.
1.1 AFISA TARAFA – (NAFASI 145)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika
mikoa kama ifuatavyo:
Arusha (nafasi 4) , Dodoma (nafasi 11), Dar es Salaam (nafasi 1), Iringa (nafasi 3),
Kagera (nafasi 3), Kigoma (nafasi 7), Kilimanjaro (nafasi 12), Lindi (nafasi 11),
Manyara (nafasi 7), Mara (nafasi 1), Mbeya (nafasi 8), Morogoro (nafasi 3), Mtwara
(nafasi 9), Mwanza (nafasi 5), Pwani (nafasi 6), Rukwa (nafasi 12), Ruvuma (nafasi
14), Shinyanga (nafasi 8), Singida (nafasi 4) Tabora (nafasi 6) na Tanga (nafasi 10).
2
1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.
Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.
Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake
Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Sheria,Menejimenti,Utawala,Sayansi ya Jamii, Kilimo, Mifugo,Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
1.1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
3
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu chuo au chuo kikuu. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka/kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Cheti cha kuhitimu mafunzo ya kompyuta
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Noveba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. WAAJIRI WOTE WALIOTAJWA HAPO JUU WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE (WILAYANI NA TARAFANI).
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Mei, 2012xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Kila mwombaji mwenye sifa aonyeshe katika barua yake mkoa anaopenda kufanyia kazi. HATA HIVYO UAMUZI WA MWISHO NI WA SEKRETARIETI YA AJIRA
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Secretary AU Katibu
Public Service Recruitment Sekretarieti ya Ajira katika Secretariat, Utumishi wa Umma
P. O. Box 63100 S. L. P 63100,
DAR ES SALAAM. DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment