Kombe la dunia la mwaka 2014, linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 12 Juni hadi Julai kumi na tatu.
Itakuwa mara ya 20 kwa kinyang’anyiro hicho kuandaliwa huku ikiwa mara ya kwanza kufanyika nchini Brazil tangu mwaka 1950 wakati wenyeji waliposhindwa na Uruguay kwenye fainali.
Ijumaa hii mbivu na mbichi itajulikana na itakuwa itakuwa wakati wa kujua nani atacheza na nani katika kundi gani droo zitakapofanyika.Itakuwa mara ya 20 kwa kinyang’anyiro hicho kuandaliwa huku ikiwa mara ya kwanza kufanyika nchini Brazil tangu mwaka 1950 wakati wenyeji waliposhindwa na Uruguay kwenye fainali.
Droo yenyewe itafanyika kuanzia saa moja jioni saa za Afrika Mashariki Ijumaa tarehe sita.
Itafanyika mjini Costa do Sauipe mkoani Bahia, umbali wa maili 56 kutoka mjini Salvador, mji utakaokuwa mwenyeji wa kombe hilo.
Wakati wa droo kutakuwa makundi manne
La kwanza likiwa na timu hizi: Brazil, Spain, Argentina, Belgium, Colombia, Germany, Switzerland, Uruguay.
Kundi la pili: Ivory Coast, Ghana, Algeria, Nigeria, Cameroon, Chile, Ecuador.
Kundi la tatu: Japan, Iran, South Korea, Australia, United States, Mexico, Costa Rica, Honduras.
Kundi la nne: Bosnia-Hercegovina, Croatia, England, Greece, Italy, Netherlands, Portugal, Russia, France.
Watakaofanya droo ni mchezaji wa zamani wa England Sir Geoff Hurst, Zinedine Zidane wa Ufaransa, Cafu wa Brazil na Fabio Cannavaro wa Italia.
Timu 32 zilizofuzu zitawekwa katika makundi manane kila kikundi kikiwa na timu nne.
0 comments:
Post a Comment