HISTORIA YA KABILA LA WANDENGEREKO
Wandengereko wanapatikana wilaya ya Rufuji kabla ya kuanza kuwaelezea wandengereko ngoja tuijue rufiji japo kwa kifupi.
Asili yao ni wilaya ya Wilaya ya rufiji ina ukubwa wa kilometa za mraba 33,539. Wilaya ya rufiji ina kata 19, kata hizo ni kama ifuatavyo Bungu, Chumbi, Ikwiriri, Kibiti,
Kiongoroni, Mahenge, Maparoni, Mbuchi, Mbwara,Mchukwi, Mgomba, Mkongo, Mtunda, Mwasemi, Ngorongo, Ruaruke, Salale na Umwe.
Wilaya ya rufiji ni moja wapo ya wilaya sita za mkoa wa Pwani ya Tanzania. Upaande
wa kaskazini imepakana na wilaya ya Kisarawe na Mkuranga na kwa upande wa
mashariki imepakana na bahari ya Indi pia kwa upande wa kusini imepakana na wilaya ya Lindi na upande wa Magharibi imepakana na mkoa wa Morogoro. Pia wilaya ya
Rufiji ina tarafa sita ambazo ni Ikwiri, Kibiti, Kikale, Mbwera, Mkongo na Mohoro.
na Rufiji, mkoa wa Pwani. Wandengereko wanatokana na wamatumbi ambao baadae
waligawanyika wengine wakafata bonde la mto Rufiji ambao wanajiita warufiji,
wengine wakaenda maeneo ya Ikwiriri, hao wakajiita wagongo ambao walikwenda
maeneo ya Mkongo na Nyambunda ambao ndio hao wandengereko.
Mavazi yao kwa asili, wanaume hupenda kuvaa Kofia, Msuli na baraghashia, wakati
wanawake wanapenda kuvaa kaniki na vilemba kichwani. Mila za zamani kabla ya
kuingiliana na imani za kidini na makabila mengine, wanaume walikuwa wakikaa
mahali peke yao na wanawake walipita mbali na mahali walipokusanyika wanaume.
Kabila la wandengereko kwa miaka mingi linasifika kwa kupenda kuvaa nguo za kaniki.
Kwa karne nyingi, vyakula vyao vya vikuu vilikuwa ugali wa muhogo, mtama ama wa
mahindi lakini ugali wa muhogo kwa karne nyingi ndio kilikuwa chakula chao kikuu.
Wandengereko ni mahiri katika kupika wali kwa nazi, na wanatumia chakula hicho
wakati wa sherehe, misiba , ngoma za asili na baada ya jando na Unyago. Ndoa za
Binti anapochumbiwa , mara nyingi aliyepeleka taarifa wa kwanza ni bibi ambaye
alikwenda kwa baba mzazi wa binti na kumweleza kwamba mwanae amepata mchumba.
Wandengereko wanajishughulisha sana na mazao ya vyakula kama vile mpunga, mahindi, mihogo n.k
ITAENDELEA BAADAE KIDOGO KAMA NI MTU WENYE ASILI YA RUFIJI ENDELEA KUPITIA UKURASA HUU KWANI UTAJIFUNZA NA KUFAHAMU MENGI KUHUSU RUFIJI NA MAKABILA MENGINE YA PWANI
0 comments:
Post a Comment