mwanazuoni

ALGERIA YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZI

Abiria mmoja alinusurika ajali hiyo iliyohusisha ndege aina ya Hercules C-130 iliyoanguka katika eneo la milima ya Oum al-Bouaghi, ikiwa njiani kuelekea mji wa Constantine.
Taarifa zinazohusiana

Afrika

Ripoti zinasema hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hiyo ya ndege.

Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika amewasifu wanajeshi waliopoteza maisha yao na kuwataja kama wafia dini wa taifa hilo.

Wengi wa abiria sabini na nane waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni maafisa wa kijeshi na familia zao.

Mwanajeshi aliyenusurika, anaripotiwa kuendelea kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Constantine baada ya kupata majeraha ya kichwa.

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa imeunda tume maalum kuchunguza ajali hiyo na kuwa Ahmed Gaid Salah, ambaye ni mkuu wa majeshi na naibu waziri wa Ulinzi atazuru eneo la ajali hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, wizara ya ulinzi imesema kuwa hali mbaya ya anga iliyohusisha kimbunga na mvua kubwa ya barafu ilisababisha ajali hiyo.

Runinga ya taifa ilionyesha picha za ajali hiyo.

Awali maafisa wa Ulinzi na shirika hilo la habari waliripoti kuwa watu 103 walikuwa ndani ya ndege hiyo lakini idadi hiyo ilipunguzwa hadi watu sabini na nane.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment