mwanazuoni

QUR AN YACHANWA VIPANDE VIPANDE






Imam ameripoti kuwa watu wanne waliokuwa wamefunika nyuso zao waliingia msikitini , wakachana nakala za Koran na kuzitupa chooni.




Polisi walifyatua mabomu ya kutolea machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa na jazba, na mtu mmoja aliuawa, duru za polisi zilieleza.

Mauritania ni taifa la kiislam , likiwa na idadi ndogo ya wakristo.

Imekuwa mshirika muhimu wa nchi za magharibi katika kampeni dhidi ya al-Qaeda na makundi mengine ya wanamgambo yanayoendesha harakati katika kanda hiyo .

Mwandishi wa habari Hamdi Mohamed El Hacen aliyeko mjini Nouakchott anasema waandamanaji walichoma vizuizi na maduka mengi na masoko yalifungwa jana siku nzima.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika kati kati mwa mji mkuu na nje ya msikiti wakipaza sauti "Mungu ni mkuu" wakidai wahusika wakamatwe na kuhukumiwa kifo kwa madai ya kukufuru uislam, alisema.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment