mwanazuoni

WATANZANIA TUITAZAME CHADEMA KWA JICHO LA TATU

WATANZANIA TUITAZAME CHADEMA KWA JICHO LA TATU

Awali ya yote napenda kumshukuru mungu kwa kuweza kunipa afya tele na kuweza kunifikisha siku nyingine na kwa mara nyingine kushika tena karamu ya wino kuandika makala hii. Hakika haya ni mawazo na fikra zangu ila ni chachu kwa watanzania makini na wenye uzalendo na nchi yake.
Tanzania ndio nchi pekee ndani ya Afrika na hata nje ya mipaka ya Tanzania kuwa na amani ya kudumu. Ni nchi ambayo watu wake wanaishi kwa amani na upendo na bila ya kubaguana na kutojali rangi , kabila na maeneo wanapoishi. Ni kiwa mtanzania mabaye anajivunia kuwa mtanzania kwa kuwa ni nchi ambayo ina amani na upendo pia inafata mfumo wa vyama vingi kwa demokrasia ya kweli.
Baada ya kuangalia utangulizi kidogo napenda sasa kwenda kwenye lengo muhimu ambalo limenifanya kuandika makala hii, kwanini nasema watanzania tuitazame CHADEMA kwa jicho la tatu? Kunasababu mbalimbali ambazo zinanifanya kusema kuwa watanzania tuitazame Chadema kwa jicho la tatu kwahiyo sababu hizo ni kama ifuatavyo: -
Kwanza suala la Udini. Usuala la udini tunatakiwa kulitazama kwa makini na bila ya woga wowote juu ya kulishughulikia jambao ili kwani ni hatari katika kudumisha amani ya nchi ambayo tumeachiwa na waasisi wetu ambao walitumia muda wao mwigi katika kutengeneza ila sisi kama atutakuwa makini juu ya suala ili tutatumia muda wetu mdogo katika kubomoa amani tulionayo. Amani ambayo tunajivunia leo watanzania ipo mbioni kupotea mithili ya machozi ndani ya maji tusipofumbua macho na kutazama suala la udini kwa makini. Tumeona au kusikia matukio ya udini ambayo yanaendelea katika nchi yetu kwa mfano kuchumwa kwa msikiti Tunduma , kuuliwa kwa Padri Geita, kuchomwa kwa Kanisa Zanzibar pia kutokea kwa mlipuko katika kanisa la Arusha. Haya ni matukio machache ambayo ni hatari kwa amani ya nchi yetu., matukio yote haya yana sura ya udini, kwani vita ya udini haina mshindi pia upelekea amani na upendo kutokomea kabisa. Mfano mzuri nchi ya Ivory Coast, nchi ambayo ilikuwa na amani ila leo imebaki kuwa historia ndani ya nchi yao. Endapo watanzania tusipoanagalia suala ili la udini kwa makini tutakuja kumtafuta mchawi ni nani. Kwanini nainasibisha suala la udini na Chadema. Kwanza ni muungano kati ya chadema na chama cha kanisa cha Ujerumani kinachoitwa Christian Development Union (CDU) kwa kuwa nchi yetu sio ya kidini sasa kwa nini chama chetu cha siasa kiwe karibu na chama cha kanisa ? kwa nini chama chetu cha siasa kiwe na mlengo sawa na chama cha kanisa ? hii nin dalili tosha kuwa kuna agenda ya siri kati ya Chadema na Kanisa hivyo watanzania tusipofumbua macho kwa kuitazama chadema kwa jicho la tatu tutakuja mkutafuta mchawi wetu hali ya kuwa tumejitakia wenyewe. Pili nainasibisha chadema na udini kwa kutazama matukio machache kama ushahidi wa juu ya ili ambalo mimi naamini ni udini. Kulipotokea tukio la bomo la Arusha kabla ya serikali ijatoa tamko tayari kuna kiongozi mmoja wa chadema pia ni mbunge alikuwa wakwanza kusema kuwa tukio la bomo ilo limesababishwa na waislamu bila hata kufanya uchunguzi juu ya ili kwa maana kuwa alikuwa anapanga kujenga chuki zidi ya waislamu na wakristo. Kwa kuwa serikali yetu makini ilifanya uchuguzi na kugundua kuwa tukio ilo alikufanywa na waislamu kwa mshitakiwa namba moja alikuwa ni kijana wa kikristo aliyejulikana kwa jina la Victa Ambros. Pia baada ya tukio ilo tulishuhudia tena bungeni mbunge wa chadema akitoa tuhuma za kumshutumu kuwa rais ni mdini kwa kuwa anawapendelea waislamu kwa lengo la kuwaaminisha wakikristo kuwa waislam pekee ndio wanapendelewa katika nchi hii ili chuki hiyo ije kuwa ni chanzo cha udini. Ila kwa kuwa kuna wabunge wazalendo wa nchi hii waliweza kuzima uzushi huo na hatimaye jaribio lingine la chadema kueneza chuki ya udini ilishindikana.

Pili suala ubaguzi. moja wapo ya sababu ya machafuko mengi dunia ni suala la ubaguzi kwani kwa wale ambao wafatiliaji wazuri wa historia ya afrika na duniani kwa ujumla ni mashahidi tosha kuwa miongoni mwa vitu ambavyo vilipelekea kutokea kwa machafuko ni ubaguzi bila ya kujali ni ubaguzi wa aina gan?, watanzania tunatakiwa kutofumbia macho suala la ubaguzi. mfano nchini Afrika Kusini moja ya kuchelewa kuapata uhuru wake ni suala la ubaguzi wa rangi ( apartheid policy), ubaguzi ambao uliutesa sana nchi ya Afrika Kusini hadi leo kuwa katika vitabu vya historia duniani kote. Leo hii suala la ubaguzi ilimeanza kushika kujitokeza kwa kasi kiasa kitu ambacho watanzania tusipokuwa makini juu ya suala hili litapelekea watanzania kupoteza amani ambayo leo tuna jivunia. Chadema ni waasisi wa ubaguzi ndani ya taifa ili kwani wameanza kudai kuwa na sera ya majimbo ambayo itapelekea kuwa bagua watanzania kwa kuwa wake katika makundi kitu ambacho ni kipya ndani ya taifa ili. Kwa leo hii mtu hana uhuru wa kwenda kukote anapopataka bila ya kuulizwa ni mzaliwa wa wapi na bila hata kujali rangi au dini na hata pia eneo alipozaliwa. Tarehe 13 April 2012, mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema alitoa tamko la ubaguzi wa dhahiri mbele ya hadhara kwa kusema kuwa Kaskazi tunataka kuwa nchi yetu ambayo rais Dr Jakaya Kikwete atakapotaka kwenda kutembelea lazima awe na pass ya kusafiria ( Passport). Walipoulizwa viongozi wa juu wa chadema juu ya tamko ilo la mbunge kijana huyo walisema kuwa ni utoto lakini mpaka leo hakuna hatua ya kinidhamu ambayo imechukuliwa juu yake hivyo kwa mtazamo wangu na fikra zangu ni kuwa mbunge huyu alisikia haya maneno katika moja ya vikao vyao vya chama kwa kuwa alikuwa hana koromeo kama waswahili wanavyosema akajituta anasema kabla ya muda kufika . Kama ubaguzi wa maeneo hautoshi Chadema wakahamia katika vyombo vyetu vya habari kuwa watanzania kusiangalie TBC mara gazeti la Mwananchi, rai na Mtanzania, uhuru ni vibaraka vya CCM na Msaliti Zitto Kabwe. Huu ni ubaguzi mwingine wa wazi kabisa hivyo watanzania tusipokuwa makini na kuitazama chadema kwa jicho la tatu watupeleka katika janga kama la Sudan au Somalia. Licha ya kuona watanzania bado ni wagumu kuwaamini ni sera yao ya uchaguzi. Ila kwa kuwa dhambi ya ubaguzi ni kuwa na kama mwalimu Nyerere aliposema kuwa “ aliyezoea kula nyama ya watu ataendelea kula nyama ya watu”. Hivi karibuni baada ya watanzania kuwa makini na kutoipokea sera yao ya Chadema ya Ubaguzi wakaamua sasa kumbagua ndugu yao wa damu na tumbo moja Zitto Zuberi Kabwe . kwani Katibu mkuu wa chama cha chadema alitamka hadharani kupitia vyombo vya habari kuwa wanachadema watakiwi kuhudhuria katika mikutano ya Zitto, huu ni ubaguzi kama wameweza kumbagua ndugu yao wa damu je watashindwa kutubagua watanzania wa Kusini, Kigoma , Pwani, Bagamoyo , ilala ,Temeke , Kinondoni? Watanzania tuwatazame hawa kwa jicho makini .
Tatu ni Uchu wa madaraka. Pia uchu wa madaraka ni mojawapo ya sababu ya kuhatarisha amani katika nchi. Mfano mzuri tumeshuhudia kwa kusikia au kutazama kinachoendelea Misri, Libya na sehemu nyingine dunia. Endapo tuankuwa na viongozi ambao wana uchu wa madaraka tutalajie siku moja Tanzania kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kama ilivyo tokea nchini Libya kwa Kiongozi wangu wa Afrika marehemu Gaddaf, alikuwa ni kiongozi mzuri na mchapa kazi alkini kwa kuwa alikuwa na uchu wa madaraka ndio uliompoza kupelekea kifo cha kizahiri kama kile ila asingekuwa na uchu wa madaraka naamini Gaddaf angezikwa kama alivyozikwa marehemu Nelson Mandela na Libya ingekuwa nchi ya kihistoria. Sasa turudi katika chama changu cha Chadema kwani migogoro yote ambalo imewahi kutokea ndani ya Chadema na inayotokea ndani ya chadema ni kwa sababu tu ya uchu wa madaraka ya viongozi wa Chadema. Ngoja tukumbushane kidogo mgogoro wa Chacha Wangwe wa mwaka 2006 ulisabaishwa na nia yake ya kutakuwa mwenyekiti wa chadema taifa. Pia mgogoro wa Zitto Kabwe ulianza pale tu alipokuwa na nia na dhamira ya kweli ya kumkomboa mtanzania kwa kutaka kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa mwaka 2009. tujikumbushe kidogo maneno aliyoyasema mwenye Zitto juu ya ili “ kwani kuna ubaya gani mwenyekiti wa chama akatokea Kigoma….? ” tunaona kuwa ndani ya chadema kuna viongozi ambao wao wanaamini ni chama chao na wamezaliwa kuongooza je ? kama tasisi ndogo ya chama wanashindwa kutumia au kuruhusu demokrasia itumike je hawa tukiwapa nchi watakubali kutoka madarakani? Kama wanatumia pesa nyingi na mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa yule ambaye anataka kuwa mwenyekiti katika chama wanampoteza kwa njia yoyote je kwa wanaharakati wazalendo wan chi hii watapona kweli? Kama endapo watanzania atutakuwa makini katika kuitazama Chadema kwa jicho la Tatu sita shangaa kuiona Tanzania tunakuwa kama Misri au Libya. Hivyo watanzania tuitazame Chadema kwa jicho la tatu na kwa umakini mkubwa bila ya wonga.

Kuna mengi ambayo tunatakiwa watanzania kuitazama Chadema kwa jicho la tatu ila kwa kuanza tutazama haya. Hivyo basi ndugu zangu watanzania wezangu tupo katika kipindi cha mchakato wa katiba mpya hivyo tuwe makini na wanasiasa , tuwatazama kwa macho mawili bila ya kupepesa macho kwani wengi ni ndumi la kuwili wapo kwenye uga wa siasa kwa lengo lao binafsi isije ikatokae kisu kukata kisu.

TUKIWATAZAMA VIBAYA WAKIFANYA VIBAYA TUSISEME VIBYA
ASANTENI


Mwandishi wa Makala
Jina: Mshana Junior
Simu namba : 0712474810
Barua pepe: halfanm8@gmail.com
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. UMEONGEA PUMBA TU BRO HUJATHIBISHA MAMBO GANI YANAPELEKEA YOTE HAYO KAMA SI CCM?

    ReplyDelete