Kiongozi wa serikali ya Libya
inayotambuliwa kimataifa, Abdullah al-Thinni amesema ana matumaini ya
kutia saini ya makubaliano ya kugawana madaraka na wapinzani wake wa
kisiasa.
Hali ya usalama nchini Libya imekuwa tete tangu wanamgambo walipoudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo,Tripoli, mwaka jana na kuweka Bunge lao.
Al-Thini ni Waziri mkuu katika Serikali iliyoweka makao yake katika eneo la mashariki ya mji wa Tobruk.
Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini humo amekuwa akifanya jitihada za kuhakikisha kuwa pande hizo mbili hasimu zinaunda Serikali ya umoja wa kitaifa.
chanzo : bbc swahili
0 comments:
Post a Comment