mwanazuoni

RAIA ZAIDI YA 28 WAUAWA NCHINI YEMENI

Raia wapatao 20 wameuawa katika mji wa Aden mapema leo kutokana na shambulio lililofanywa na waasi wa kuhouthi nchini Yemen. Na kwa mujibu wa taarifa ya hospitali, watu wengine 41 walijeruhiwa

 Mtambo wa kuchakachua mafuta chashambuliwa


Waasi wa kihouthi na washirika wao waliitwanga kwa roketi zaaina ya Katyusa wilaya ya al-Mansura inayoshikiliwa na wanaoiunga mkono serikali.
Msemaji wa majeshi yanaoitii serikali amearifu kwamba waasi hao walizifyatua roketi 15 kutokea kwenye ngome yao ya Dar Saad . Msemaji huyo Ali al-Ahmad ameeleza kuwa mashambulio hayo ya makombora yalianza majira ya mapambazuko wakati ambapo pilipilika zinaanza.
Kwa mujibu wa taarifa watu wengine waliokuwa mazikoni pia walishambuliwa kwa makombora. Watu hao walikuwa wanawazika raia wengine waliouawa hapo awali kutokana na shambulio jingine la makombora. Duru za hospitali zimeliambia shirika la habari la AFP kwamba waliojeruhiwa wamo katika hali mbaya.
Mji wa Aden ulikuwa kituo cha mwisho ambako Rais Manosour Hadi alikimbilia kabla ya kupata hifadhi katika nchi jirani ya Saudi Arabia. Rais Mansour Hadi alikimbilia Saudi Arabia mnamo mwezi wa Machi na majeshi yanayomtii yameendelea kupambana na waasi kwa kuungwa mkono na vikosi vya anga vya mfungamano wa kijeshi wa nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia.
Gereza lafunguliwa
Wakati huo huo waasi wanaoyakimbia majeshi ya serikali waliiteka jela moja iliyoko kusini magharibi mwa Yemen na kuwafungulia wafungwa wapatao 1200. Waliofunguliwa walikuwa pamoja na wafungwa waliohukumiwa kwa mauaji ya kudhamiria.
Waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wameyatwaa maeneo makubwa nchini Yemen tangu waanzishe mashambulio mnamo mwezi wa Julai, mwaka uliopita. Licha ya mazungumzo ya amani mjini Geneva pamoja na mashambulio ya ndege yanayoongozwa na Saudi Arabia, bado haijawezekana kuwatimua waasi hao, na bado wanaendelea kupambana na majeshi ya serikali ya Yemen.
Shirika la habari la Saba linalodhibitiwa na waasi wa Kihouthi pia limearifu kwamba waasi waliishambulia kwa kombora, kambi ya kijeshi ya Al-Salil katika jimbo la Riyadh ndani kabisa ya ardhi ya Saudi Arabia.
Msemaji wa waasi alinukuliwa akisema kwamba shambulio hilo lilifanywa mapema jana ni ujumbe kwa wakandamizaji wa Saudi Arabia.
Lakini Saudi Arabia imekanusha kushambuliwa kwa kombora hilo aina ya Scud. Msemaji wa serikali ya Saudi Arabia ameeleza kwamba wao hawana habari juu ya shambulio hilo.Amesema hakuna sehemu yoyote ya ardhi ya Saudi Arabia iliyoharibiwa. Hata hivyo msemaji wa ulinzi wa raia amefahamisha raia wawili walijeruhiwa hapo jana kutokana na shambulio la kombora lililofyatuliwa kutokea ndani ya Saudi Arabia.
Mwandishi:Mtullya Abdu.afp,
Mhariri:Iddi Ssessanga


Chanzo: DW swahili
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment