HUZUNI YATANDA SINGIDA MJINI
Mbunge wa Singida Mjini kwa tiketi ya CCM, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena Ubunge jimboni humo wakati wa Mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida, mkutano uliofanyika katika viwanja vya People's Club.
UMATI ULIOFURIKA
Huzuni yatanda pale mbunge wa Singida mjini alipoaga rasmi kuwa atagombea tena
Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja la Kangariga wakati wa mkutano huo.
Msanii maarufu nchini, Nasbu Abdul 'Diamond Platnumz' akiingia jukwaani na wacheza shoo wake kuwapa burudani wananchi wa Singida Mjini.
0 comments:
Post a Comment