Timu ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya
wakata miwa wa Kagera Sugar katika mchezo uliofanyika kwenye dimba la
CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute, Simba walijipatia goli
lao lililofungwa na mshambuliaji kinda machachari Ibrahim Ajibu katika
dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.
Ajibu alifunga bao hilo baada ya kumalizia pasi ya kisigino kutoka kwa
Hamisi Kiiza aliyepokea pasi ya pembeni kutoka kwa Mwinyi Kazimoto.
Kagera walionekana kujitutumua lakini hata hivyo juhudi zao ziligonga mwamba.
Simba walifanikiwa kupata penati katika dakika ya 82, baada ya
mwamuzi Mathew Akrama kuamuru adhabu hiyo kutokana na Ajibu kuangushwa
ndani ya eneo la hatari na Juma Jabu, lakini hata hivyo Ibrahim Ajibu
alijikuta akikosa baada ya kipa wa Kagera Sugar kupangua mpira huo
Kagera Sugar walipata pigo zaidi baada ya Daudi Jumanne kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumtolea mwamuzi lugha chafu.
Simba inaendelea kushikilia nafasi ya pili mbele ya Azam yenye pointi
sawa lakini wekundu wa Msimbazi wakiwa uwiano mzuri zaidi wa mabao ya
kufunga na kufungwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment