WAZIRI wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry
amefanya mazungumzo na Mfalme Salman wa Saudi Arabia kuhusu mizozo ya
Syria, Libya na Yemen, kabla ya mikutano ya kimataifa inayopangwa
kuandaliwa wiki ijayo barani Ulaya kuhusu mizozo hiyo.
Ziara ya Kerry, ambaye pia amefanya mazungumzo na mwanamrithi wa
ufalme na naibu mwanamrithi wa ufalme na waziri wa mambo ya nje, inakuja
katika wakati muhimu wa kuimarisha juhudi za kudhibiti mapigano na
kuhimiza mazungumzo ya kisiasa katika nchi zote tatu ambazo zimekumbwa
na machafuko kwa miaka mingi.
Kerry anajaribu kuunga mkono mpango tete wa kusitishwa kwa mapigano
nchini Syria ambao umekiukwa mara kadhaa na pande zote za mgogoro.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment