mwanazuoni

MAUAJI YA KIMBALI

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Wadau wapenzi, moja ya istilahi za kisiasa zilizoingia katika msamiati wa kisiasa baada ya Vita vya Pili vya Dunia ni mauaji ya kimbari. Matukio yaliyojiri katika Vita vya Pili vya Dunia yaliifanya jamii ya kimataifa kulipa uzito mkubwa suala la kupambana na jambo hilo ovu. Ni kutokana na kuzingatia pia umuhimu wa kujadili suala hilo ndio maana tumeamua kukuandalieni mfululizo huu wa makala fupi fupi zitakazozungumiwa historia ya istilhi hiyo na kugusia matukio mbalimbali ya mauaji ya kimbari katika kipindi hiki chote cha baada ya Vita vya Pili vya Dunia hususan katika miongo miwili iliyopita.


Mauaji ya kimbari ni ukatili na uhalifu mbaya zaidi wa kimataifa ambao umekuwa na athari kubwa mbaya na zisizofidika kwa mwanadamu. Istilahi ya Genocide au Mauaji ya Kimbari inatokana na maneno mawili ya Kigiriki ya genos kwa maana ya mbari, kizazi au kundi la watu na caedere lenye maana ya kuangamiza, kufanya mauaji na kuua watu. Huo ni uhalifu wenye historia ndefu, lakini kwa hivi sasa imepata sura mpya kwa istilahi hiyo. Tab'an muundo wa mauaji ya kimbari leo hii unatofautiana na wa miaka mingi ya huko nyuma ya kabla ya kugundiliwa silaha za mauaji ya umati. Naam, kabla ya kugundiliwa silaha za mauaji ya umati, mtu mmoja pekee alikuwa hana uwezo wa kuua maelfu ya watu, bali alihitajia jeshi la watu wengi kumsaidia katika uhalifu wake wa kutisha. Hivyo katika karne za huko nyuma, mauaji ya kimbari yalikuwa yakifanywa na idadi kubwa ya watu dhidi ya watu wengine. Lakini cha kusikitisha ni kuwa, katika miongo ya hivi karibuni, mauaji ya kimbari yamekuwa yakifanyika kwa jina la watu wengi dhidi ya watu wa jamii ya wachache.

Vita viwili vya dunia vilitumiwa kama kisingizio na baadhi ya watu kufanya mauaji ya umati kwa kutumia taasubu za kikabila, kitaifa na rangi na kueneza chuki za kupindukia baina ya wanadamu. Ni kwa sababu hiyo ndio maana mwanasheria maarufu wa Poland anayejulikana kwa jina la Raphael Lemkin alitoa pendekezo mwaka 1933 la kuhesabiwa rasmi mauaji ya kimbari kuwa ni uhalifu. Alitoa pendekezo hilo katika mkutano wa tano wa kimataifa uliohusu haki za binadamu uliofanyika mjini Madrid, Uhispania na kupendekeza kitendo cha kuangamiza kizazi, makundi ya kidini au ya kijamii kitangazwe rasmi kuwa ni uhalifu kwa mujibu wa sheria za mataifa yote ya dunia. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia na kuasisiwa Umoja wa Mataifa, kulitolewa azimio mwezi Disemba 1946 ambalo lilitangaza kuwa mauaji ya kimbari ni uhalifu, na kwamba dunia iliyostaarabika inachukizwa mno na kitendo hicho. Baada ya kutolewa azimio hilo, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tarehe 9 Disemba mwaka huo huo likatumia azimio hilo kutoa hati maalu
Umoja wa Mataifa unazingatia vigezo kadhaa vikuu katika kuanisha neno genocide yaani mauaji ya kimbari. Kuua idadi ya watu kutoka kundi moja la watu, kuwadhuru vibaya kimwili na kiroho watu wa kundi hilo, kuharibu kwa makusudi maisha ya watu wa kundi hilo kwa ajili ya kuwaangamiza wote au baadhi ya watu wa kundi hilo, kuweka sheria za kuzuia kuzaana na kuongezeka idadi ya watu wa kundi hilo na mwishowe kuwahamisha kwa nguvu watoto wa kundi hilo na kuwapeleka katika kundi jingine la watu ni miongoni mwa vielelezo vinavyotumiwa na Umoja wa Mataifa kuainisha uangamizaji wa mbari na kizazi yaani genocide. Hivyo moja ya misingi na vielelezo vikuu vya uhalifu wa uangamizaji wa kizazi ni kwamba wahanga wa uangamizaji huo huwa wanatoka katika kundi moja maalumu la watu.
Vile vile miongoni mwa sifa kuu za uangamizaji wa kizazi ni kwamba hazihusiani tu na kuua watu kwa maelfu, bali inahusiana na malengo ya watendaji wa jinai hizo, yaani kulilenga kundi fulani la watu kwa nia ya kuliangamiza. Kuwafanya watu wa kundi hilo kuwa katika hatari ya kuuawa, kuhukumiwa kidhulma, kuporwa mali zao, kunyanyaswa, kufukuzwa katika makazi yao ya jadi na hatimaye kuuliwa kwa halaiki. Historia inaonesha kuwa, makundi ya kitaifa ni mepesi sana kuwa wahanga wa uhalifu huo. Makundi hayo hasa yale ya wachache, mara nyingi yanahesabiwa kuwa ni ya watu duni na yanaonekana ni ya watu baki hata ndani ya jamii na ardhi yao wenyewe. Kwanza watu hao wanapachikwa majina mabaya na kudaiwa kuwa ni hatari kubwa kwa nchi yao na hatimaye hufanywa shabaha ya unyanyasaji na ukandamizaji.
Licha ya kwamba baada ya Vita vya Pili vya Dunia jinai hiyo ilianza kuhesabiwa kuwa ni jinai kubwa zaidi kimataifa, lakini cha kusikikitisha ni kwamba walimwengu mara nyingi wameendeleea kushuhudia jinai hiyo ikitokea katika kona mbalimbali za dunia. Mwishoni mwa muongo wa sabiini, walimwengu walishuhudia mauji ya kimbari yaliyofanywa na jeshi jekundu huko Cambodia. Walimwengu walishuhudia pia mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Wahutu dhidi ya Watutsi na dhidi ya Wahutu wenye misimamo ya wastani nchini Rwanda katika muongo wa 90, mauaji yaliyofanywa na Saddam dhidi ya Wakurdi na Mashia nchini Iraq katika miongo ya 80 na 90, mauji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina huko Sabra na Shatila pamoja na mauaji ya kimbari ya hivi karibuni huko Ghaza, kuuliwa kwa umati Waislamu wa Bosnia Herzegovina, mauaji ya umati yanayofanywa na mabudha dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar na mauaji mengineyo. Hiyo ni sehemu ndogo tu ya jinai kubwa zinazofanyika kwa jina la siasa za mauaji ya kimbari katika maeneo mbalimbali duniani. Tutaendelea mbele na makala hii katika sehemu ya tatu ambapo tutatupia jicho nafasi ya jamii ya kimataifa katika suala hilo, Inshaallahmu ya kupiga marufuku na kumwadhibu kila atakayepatikana na hatia ya kufanya mauaji ya kimbari. Kila taifa duniani liliwajibishwa kutekeleza vipengee vya hati hiyo kuanzia tarehe 12 Januari 1951.   vigezo vinavyotumiwa na Umoja wa Mataifa kubainisha maana ya mauaji ya kimbari na tutakhitimisha sehemu ya leo ya makala hii kwa kutoa mifano ya mauaji ya kimbari yaliyotokea ulimwenguni. Karibuni.


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment