Vikosi vya ulinzi na usalama Dar es salaam vimekamata mifuko ya sukari
katika ghorofa linalojengwa maeneo ya Kinondoni baada ya kuripotiwa
kufichwa na mfanyabiashara mwenye asili ya asia.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda pamoja na mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Hapi walifika kwenye eneo.
Mmiliki
wa jengo hili amesema sukari hiyo sio ya biashara bali ni kwa ajili ya
misaada na amekua akiwapa watu ambapo pamoja na majibu hayo Makonda
ameagiza jeshi la Polisi kuendelea kumhoji.
0 comments:
Post a Comment