CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.
Uamuzi huo unatokana na kikao cha Kamati Kuu kilichoketi mjini hapa kwa siku mbili.
Akizungumza
na waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu Zazinzar, Salum Mwalimu
alisema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, Mwenyekiti wa chama,
Freeman Mbowe ana mamlaka ya kuteua majina sita ya wajumbe wateule.
Alisema
katika kikao hicho mambo mengi yamezungumzwa lakini pia kuna mambo ya
kimkakati hasa katika kuelekea kumaliza mwaka huu na kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa na hata uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Mwalimu
alisema katiba yao ya mwaka 2006, inazungumzia wajumbe wateule wasiozidi
sita ambao watapendekezwa na mwenyekiti wa taifa kwa kushauriana na
katibu mkuu na kuridhiwa na vikao.
Alisema Mwenyekiti wa taifa wa
chama hicho ametumia kipengele hicho kupendekeza jina la Sumaye kuwa
mjumbe wa kamati kuu na jina hilo liliungwa mkono na kikao na kuafikiwa
na kamati kuu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment