Zlatan Ibrahimovic bado hajapokea ofa rasmi ya mkataba kutoka kwa
Manchester United, wakala wake amethibitisha usiku wa kuamkia leo.
Mapema leo, siku kadhaa kabla ya Ibrahimovic kuichezea Paris Saint
Germain mchezo wa mwisho, Radio RMC France imeripoti kwamba United
tayari wameshampa mshambuliaji huyo wa Sweden mkataba wa mwaka mmoja.
Lakini wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola alionge na Sky Sports News na kukanusha taarifa hizo.
“Kwenye dunia ya sasa inabidi tukubaliane na ukweli kwamba kuna
baadhi ya waandishi wa habari hutengeneza story – hii sio taarifa ya
kweli,” alisema Raiola.
RMC Radio ndio kituo cha habari ambacho kwa mara ya kwanza walianza
kuripoti usajili wa mshambuliaji Anthony Martial kutoka Monaco kwenda
Man United, leo waliripoti kwamba tayari United wamempa ofa ya mkataba
wa mwaka mmoja Zlatan kujiunga nao mara Jose Mourinho atakapopewa timu
kuiongoza.
Ibrahimovic Alithibitisha Ijumaa iliyopita kwamba angeondoka PSG
mwishonu mwa msimu na kuna baadhi ya taarifa zinasema amekuwa kwenye
mazungunzo na LA Galaxy japo uhamisho huo utakuwa mgumu kutoka na Galaxy
kubanwa na kanunj za usajili kwa kumuongeza Zlatan, hivyo itawabidi
wasubiri mpaka mwaka 2017 ili kufanisha usajili huo.
Ibrahimovic ataitumikia PSG kwenye mchezo wa mwisho kwenye fainali ya kombe la Ufaransa dhidi ya Marseille.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment