mwanazuoni

PICHA YA BISMINI IONDOLEWE IWEKWE YA DIAMOND

View attachment 348239

Wandugu huyu Mbunge ameonekana kituko.kituko kwa kutaka Diamond awekwe badala ya Picha ya askari ...nadhani ni utoto zaidi..Ila mimi nimeona hoja yake inaibua mjadala mpana kuhusu picha ile na Tanganyika.
Jee sanamu ile ni ya nini ?
Huyu mbunge ametufunua wengi kuhusu ile sanamu.
Ni sanamu ya askari wa malkia wa UK alopigana kumuondoa mzungu mwenzie wa Kijerumani. Yule ni mwafrika , mwafrika alotumiwa na wakoloni hivyo nawwza kumwita alikua upande wa wakoloni ...wapo askari wabeba miziko au wapagazi walo andikwa katika placard ya pale. Lakini hawa sio mashujaa wa Tanganyika hata kama ni waafrika...hawa walipigana upande wa mkoloni muingereza dhidi ya mkoloni mjerumani hawa ni puppets sio wazalendo.
Naibua mjadala huu kwa makusudi na mbunge yule amechokonoa hoja ya msingi kabisa japo yeye kaleta uchepe.

Wafrika wa nchi hii walopambana na wakoloni ni Kinjekitile, Chief Mkwawa, Bushiri.
Hawa walipoteza maisha yao kuilinda Tanganyika dhidi ya Ukoloni hawa wanastahiki kabisa stutue zao kusima pale tena za dhahabu ...na mtag ndugu yangu Mwanahistoria Mohamed Said aje nae atie mchango wake kuhusu hili..
Wakoloni walitufanya wanaserere hata historia zetu tukazitia kwenye kapu na kutukuza za kwao.

Mwanzo ilikua picha ya askari wa kijerumani Major Hermann von Wissmann Waingereza waliindoa pamoja na Ya Bismack na Karls Peter

Sanamu Hii ya sasa , Ilizinduliwa Rasmi Dar es salaam hapo ilipo Mwaka 1927. Sanamu Hii imetengenezwa kwa shaba na imechongwa na James Alexander Stevenson.

Kabla haija letwa Dar es salaam iliwekwa kwa maonesho katika Royal Academy , London.

Tujaribu kusoma historia , kama hujui historia ya sanamu ile unakua saw ana huyo Mbunge . Hapa tunatakiwa kuijadili ile sanamu kama jee ibaki kama ilivo ambapo askari Puppet alo pigana upande wa Mfalme wa Uingereza dhidi ya Kals Peter wa Ujerumani ina maana yoyote Kwetu.

Jee si wakati mzuri wa kuwaenzi Kinjekitile, Abushiri na Mkwawa walopigana dhidi ya Ukoloni ? Hii ni hoja moto

Hii ni mada moto , hard talk kila mtu ajadili hili .
Bi. Maunda Plantan mjukuu wa Affande Plantan akimsomesha Mwandishi historia ya wazee
wake katika Tanganyika. Bi. Maunda alikuwa mwalimu na mtangazaji wa kwanza wa kike
Tanganyika Radio Dar es Salaam ilipoanzishwa nwaka wa 1952


Macos,
Ahsante sana kwa kunitaja katika hii mada ya Picha ya Bismini na kuniomba nichangie. Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1914 - 1918) Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Wajerumani. Sanamu hii ya Bismini ni kwa ajili ya kuwakumbuka askari wa waliopigana upande wa Muingereza dhidi ya Mjerumani.
Hii ni kumbukumbu ya babu zetu askari na wapagazi Waafrika ndani ya jeshi la Muingereza. Kama ulivyosema ni kuwa awali ilikuwapo picha ya Herman Von Wissman. Huyu Wissman ndiye aliyeongoza vita dhidi ya wananchi wa Tanganyika kwa kuleta askari mamluki Wanubi kutoka Sudan na Wazulu kutoka Mozambique.
Katika hawa Wanubi maarufu katika askari hawa katika mji wa Dar es Salaam ni Mzee Hamisi baba yake Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African Association pale ilipoanzishwa mwaka wa 1929. Mtoto wa Ibrahim HamisiAbdallah Ibrahim ni mmoja wa watu niliozungumza nao katika kujifunza historia ya mji wa Dar es Salaam.
Askari wengine walitoka Congo na mmoja wapo ni babu yangu mkuu Samitungo Mwekapopo aliyekuwa katika Boma la Wajerumani Shirati, Musoma. Katika Wazulu walioingia Tanganyika pamoja na Wissman ambao taarifa zao ziliweza kuhifadhiwa ni Sykes Mbuwane baba yake Kleist Sykes, baba yao Abduwahid, Ally na Abbas Sykes.
Hawa askari wote mamluki walikuwa katika kikosi kilichojulikana baadae kama ''Germany Constabulary,'' na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan baba yao Mwalimu Thomas Saudtz Plantan, Schneider Abdilllah Plantan, na Ramadhani Mashado Plantan.
Wakati wa Vita Vya Pili Mwalimu Thomas Plantan ndiye alikuwa rais wa African Association. Inasemekana huyu Affande Plantan alikuwa ndiye chifu wa Wazulu Mozambique na ndiye aliyewekeana mkataba na Wissman kuja na jeshi la Wazulu kuiteka Tanganyika. Mamluki hawa wa Kizulu walikuja na meli ya  kivita ya Wajerumani hadi Pangani. Hapo ndipo yalipoanza mapambano yao na Abushiri na baada ya kukamatwa Abushiri ndipo jeshi likaelekea Kalenga kwa Chifu Mkwawa.
Katika mswada wa kitabu alichoandika Kleist Sykes (1894 - 1949) kuhusu maisha yake, Kleist anaeleza kuwa mkataba ulikuwa Wazulu na Wajerumani kuitawala Tanganyika kwa ushirika. Wazulu na ujuzi wao katika medani ya vita uliwawezesha Wajerumani kuwashinda Abushiri bin Salim na Chifu MkwawaWajerumani ndiyo katika kuonesha shukurani yao kwa Wazulu walimfanya Affande Plantan kuwa mkuu wa majeshi yao na wakaliita jeshi hilo ''Germany Constabulary.'' Haya kaeleza Kleist katika mswada wake.
Vilevile waliwajengea shule watoto wa wanajeshi wao ambayo ilikuwa ilipo sasa Ocean Road Hospital ambako Kleist alisoma hapo hadi darasa la sita na alipomaliza akaingizwa katika jeshi pamoja na Schneider.
Wakati wote wa utawala wa Wajerumani Waafrika hawa wakiishi ndani ya kambi ilikuwatenganisha na wazalendo wa Tanganyika kwa falsafa ile ile ya wakoloni. Wagawe uwatawale.
Kwa hali hii ya kutoa elimu kwa watoto wa askari katika jeshi la Wajerumani, hawa wakoloni walifanikiwa kuwanyanyua juu Wazulu na Wanubi kiasi kuwa waliposhindwa Vita Kuu ya Pili na Waingereza kuja sasa kuitawala Tanganyika, walioweza kupata kazi za maana katika utawala mpya walikuwa hawa Wazulu na Wanubi ingawa katika vita ile walipigana dhidi ya Muingereza katika jeshi la Wajerumani.
Watoto wa hawa Wazulu walioingia Tanganyika na Wissman ambao walipigana dhidi ya Waingereza ambao kumbukumbu zao zimehifadhiwa na akina Sykes na Plantan.
Katika Vita ya Kwanza ya Dunia watoto wa hawa Wazulu walipigana chini ya uongozi wa Von Lettow Vorbeck aliyekuwa wakati ule ndiye mkuu wa majeshi ya Ujerumani Tanganyika.
Kleist ndiye alikuwa Aide de Camp wa Vorbeck.
Vorbeck alipoona kazidiwa nguvu na majeshi ya Waingereza akishambuliwa na General Smuts kutoka Afrika ya Kusini alivuka mpaka akakimbilia Mozambique na baadhi ya askari wake wa Kizulu.
Kleist alikamatwa mateka na akawekwa kambi ya askari mateka Dodoma.
Kitu cha kuangalia ni kuwa hawa watoto wa Wazulu na Wanubi ambao walipigana dhidi ya Waingereza ndiyo waliokuja kufanya mabadiliko makubwa katika siasa za Tanganyika katika kudai uhuru kutoka kwa Waingereza, uhuru ambao ni wa nchi ambayo ilikuwa yao kwa kuhamia na wengine kwa kuzaliwa.
Mathalan Mwalimu Thomas Plantan na nduguze wote hawakuzaliwa Tanganyika walikuja baada ya baba yao kuwa keshajiweka vizuri nchini.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Mashado Plantan alikuja Tanganyika mwaka wa 1905.
Hawa vijana wote wa Kizulu walikuwa katika African Association, Kleist akiwa muasisi khasa na Schneider akiwa mwanaharakati wa kupigiwa mfano kwani aliwataabisha sana Waingereza khasa wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1938 - 1945) kiasi cha Waingereza kuamua kumkamata na kumuweka kizuizini Mwanza alikofungwa hadi mwisho wa vita.
Mashado yeye alianzisha gazeti, ''Zuhra,'' na ndiyo ilikuwa sauti ya Mtanganyika wakati wa ukoloni.
Kleist ingawa alikuwa karibu sana na Waingereza yeye alijiingiza katika siasa za kuwapinga Waingereza kichinichini na alipounda African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama alichokiasisi mwaka wa 1933 na rafiki yake wa Kimanyema, Mzee bin Sudi.
Hawa vijana wa Kizulu katika Tanganyika ile ya 1930 wao wakijiona bado ni askari katika jeshi la Kijerumani na zaidi kwa kuwa wote walikuwa wakikisema Kijerumani kama maji. Hili jambo bila shaka likiwakera sana Waingereza.
Sidhani kama hawa Wazulu na Wanubi walikuwa wakikerwa na ile sanamu ya kamanda wa baba zao Hermann von Wissman.
Lakini Vita ya Pili ya Dunia ilipoingia Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally walivaa sare za majeshi ya King's African Rifles (KAR) kupigana na Wajerumani ambao walikuwa washirika wa babu na baba yao.
Abdul na Ally walikwenda kupigana Burma dhidi ya Wajapani na wote wawili walipewa medali ya ''Burma Star,'' na Waingereza baada ya kwisha vita mwaka wa 1945.
CHANZO:http://www.mohammedsaid.com/

Hizi ndizo athari za ukoloni. Kumbukumbu hizi tuzichukulie kama kumbukumbu katika historia ya Tanganyika. Soko la Kariakoo ambako ndipo Waingereza walipokuwa wakiwaandika kazi za upagazi babu zetu wakati wa vita bado lipo hali kadhalika Bismini na bunduki yake sanamu ile bado tunayo. Mimi binafsi vyote hivi havinitaabishi hata chembe navitazama kama zilivyo - historia yetu ambayo hatwezi kuikimbia hata kama tutataka.
Kuhusu Diamond...

Kwa kawaida mwanamuziki akifanya makubwa huwa anawekwa kwenye ''Hall of Fame,'' au
sanamu yake inawekwa pale alipokuwa akifanyia muziki wake. Liverpool ipo sanamu ya The Beatles na Mephis ipo sanamu ya Elvis Presley.
Sanamu ya The Beatles Liverpool

Sanamu ya Elvis Presley    
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment