mwanazuoni

FIFA YAPATA KATIBU MKUU MWANAMKE



Raisi wa FIFA SIKU ya Ijumaa alimteua mwanamama Fatma Samoura wa Senegal,  mwanadiplomasia mkongwe wa Umoja wa Mataifa kuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo.
Samoura atakuwa mwanamke wa kwanza kushika madaraka makubwa zaidi ndani ya FIFA. Ataanza kuitumikia nafasi hiyo katika mfumo mpya uliobadilishwa wa shirikisho hilo mwaka huu.
FIFA imesema Samoura anategemewa kuanza kazi June, baada kukamilishwa kwa taratibu zote za kujiridhisha na maadili ya viongozi wa juu wa FIFA.
Samoura ana uzoefu wa miongo kadhaa kwenye Umoja wa Mataifa upande wa Afrika,  zaidi akiwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwenye mpango wa Maendeleo nchini Nigeria.  Hata hivyo mwanamama huyo hana uzoefu kwenye uongozi wa michezo au kwenye majadiliano ya mauzo ya haki za matangazo ya TV na mikataba ya udhamini, mambo ambayo yatakuwa ni majukumu yake makubwa. 
Raisi wa FIFA Gianni Infatino amesema amemteua mwanamama huyo kwasabau alihitaji mtu kutoka nje ya siasa za soka na mtu ambahe ataleta upepo mpya ndani ya shirikisho hilo.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment