May 16
2016 Sakata la Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises
lilitarajiwa kujadiliwa bungeni wakati wa mjadala wa Makadirio ya Bajeti
ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamati ya
Bunge Wizara ya Mambo ya Ndani imependekeza suala la Mkataba huo
unaohusisha ufungwaji mashine za alama za vidole ‘fingerprint’
usijadiliwe bungeni na badala yake liachwe kwa kamati ya bunge ya PAC
iliyoanza kulifuatilia suala hilo lililoibuliwa na CAG katika ripoti
yake ya ukaguzi kwa mwaka 2014/15.
Mjadala wa
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani 2016/17 umeahirishwa hadi saa kumi
kamili ili kutoa nafasi kwa Kambi rasmi ya upinzani kukutana na kamati
ya kanuni ili kuipitia upya hotuba ya kambi hiyo iliyotarajiwa
kuwasilishwa kwenye kikao cha asubuhi leo hii.
0 comments:
Post a Comment